Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
We we ni mmoja wa watu wajinga kabisa duniani. Hao wazazi umeambiwa wako aged 90 + years, too old to handle such big issues bado unakuja hapa kuandika huo ujinga
 
This is the beginning of the end, sorry the end of the beginning..
 
Siku ya hukumu mwendazake hatopaswa kusomewa mashitaka aise ..yani yeye ni moja kwa moja motoni huko aendelee kuwaka tu hata sasa tuna iman yupo anaungua tu, tunaomba mkuu wa kuzimu aongeze kuni zaid na zaid kwa huyu mwendazake.

Kwanini unasema hivyo? Shida yetu ni kukosa balanced story. Ule ulikuwa uwanja wa vita. Nini hasa kilitokea na nani aliyefanya hayo?
 


04 June 2021




Baada ya kauli za kupingana kati ya ile ya waziri Prof. Palamagamba Kabudi wa serikali ya Tanzania alipohojiwa na BBC Swahili na ya msemaji wa Mkuu serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda hapo mwezi November 2017. Msemaji wa serikali Dr. Hassan Abbas alisema serikali iliyokuwa chini ya hayati rais John Pombe Joseph Magufuli inafanya jitihada zote kujua kuhusu kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda.

Wazazi wa Azory Gwanda wameomba msaada wa serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iendelee kufuatilia kujua taarifa kamili juu ya suala la kupotea mwandishi huyo wa Mwananchi Media Corporation ili ieleweke kilichompata mwandishi huyo ili wazazi na familia ya Azory Gwanda wafahamu yaliyomkuta kama bado yupo hai au amefariki .

Source : CHADEMA MEDIA TV
 
Asante mkuu 'kalonji'.

Kwa hakika "killing" haiwezi kuwa utatuzi wa kila jambo. Ni njia ya mkato ya kuondoa tatizo kwa muda, bila ya kuliondoa kwa muda mrefu.
Killing ufanywa na watu wasiojiamini,wasioelimika.
Aliyelimika ukuuwa kwa point
 
Kwa kweli inauma sana.

Nikikumbuka kupotezwa kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye, kushambuliwa kwa Tundu Lisu, kuwabbikia watu kesi za uhujumu uchumi, n.k. - sababu kubwa ni kumkosoa tu, naamini kabisa yule bwana alikuwa ni sehemu ya utawala wa shetani. Hakuwahi kumjua Mungu wa kweli, na Kanisani alienda kuwadhihaki wana wa Mungu, na siyo kufanya toba au kumwabudu Mungu wa Kweli.
Simon Kanguye alimkosoa nini Mwendazake be specific?
 
Alikuwa akifatilia unyama uliofanywa kibiti ikiwemo ukatili na mauaji ya wasio na hatia kwa kuhisiwa tu eti ni magaidi ikapelekea wengi kuumizwa japo sio wahusika.But haki za watu huwa hazipotei bure.
Killing haijawahi kuwa solution Tza sio Rwanda.
Matukio Kibiti yalikuepo au ni uzushi?

Wakazi wa Kibiti walitoa ushirikiano gani kukomesha matukio hayo?

Walitoa kwa hiari au nguvu?

Matukio yaliendelea au yalikoma?

Kwa maoni yako mbinu ipi bora ingelitumika kukomesha matukio yale?
 
Kwani mama Samia hakuwa makamu wa raisi?
Huna taarifa kwamba kuna wakati alitaka kujiuzuru? Akakataliwa? (System ilimzuia)

Unafikiri kwa nini alifikia hatua hiyo?

Umechelewa sana kumjua Jiwe.
 
Mafia wa nchi zilizoendelea ( Ulaya, Marekani na Mashariki ya Kati ) na zinazotumia Akili vyema wakifanya Tukio basi watatengeneza Mazingira wala wasijulikane kabisa kuwa ni Wao, ila Mafia wa Uswahilini ( hasa Barani Afrika ) wakifanya Tukio kutokana na ' Upumbavu / Upopoma ' wao wataliacha hivyo hivyo mpaka hata ' Mangumbaru / Wajinga ' watajua tu kuwa Wahusika ni Wao

hapa ndio namkubali jamaa yako PK, kwenye mambo kama haya huwa haachi traces kabisa ...
Wakwetu inaonekana wengi ni knovice kwenye kazi....Ona lile tukio la TL yaani ni utoto kabisa..
 
hapa ndio namkubali jamaa yako PK, kwenye mambo kama haya huwa haachi traces kabisa ...
Wakwetu inaonekana wengi ni knovice kwenye kazi....Ona lile tukio la TL yaani ni utoto kabisa..
Waje ( Wanione ) niwafanyie ' Free Consultation ' juu ya ' Matukio ' haya na hakuna Mtanzania ambaye anaweza Kuwagundua ( Kuwashtukia ) pale wakiwa wanayafanya. Huwezi ' Kupikwa ' vyema na akina Museveni na Kagame katika ' Umafia ' halafu ukawa Ngumbaru ( Mjinga ) au Popoma ( Mpumbavu )
 
Kutoweka kwa huyu mwandishi kunatatanisha kwani hata haijulikani alikuwa akiandika au akitafuta taarifa juu ya kitu gani ambacho kingeweza kuwa ndiyo sababu ya kutoweka kwake.

Hivi huko Mwananchi nao hawajui alikuwa akishughulika na habari gani?

Je kwenye magazeti ni habari zipi alizokuwa anaziandika, ili tujaribu kuunganisha doti?.

Hii ni tofauti kabisa na kutoweka kwa Ben Saanane, ambaye habarizilizosababisha apotee zinajulikana wazi.
Alikuwa anaandika na kufuatilia kisa na mikasa wa yale mauaji ya kutatanisha kule Kibiti...
 
Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
Yani we kweli hamnazo. Yani uende ukaombe msaada kwa muuaji mwenyewe?
 
Back
Top Bottom