Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Mafia wa nchi zilizoendelea ( Ulaya, Marekani na Mashariki ya Kati ) na zinazotumia Akili vyema wakifanya Tukio basi watatengeneza Mazingira wala wasijulikane kabisa kuwa ni Wao, ila Mafia wa Uswahilini ( hasa Barani Afrika ) wakifanya Tukio kutokana na ' Upumbavu / Upopoma ' wao wataliacha hivyo hivyo mpaka hata ' Mangumbaru / Wajinga ' watajua tu kuwa Wahusika ni Wao
Ndo ujue tofauti ya akili ya ndumba na akili ya darasani
 
04 June 2021

Baada ya kauli za kupingana kati ya ile ya waziri Prof. Palamagamba Kabudi wa serikali ya Tanzania alipohojiwa na BBC Swahili na ya msemaji wa Mkuu serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda hapo mwezi November 2017. Msemaji wa serikali Dr. Hassan Abbas alisema serikali iliyokuwa chini ya hayati rais John Pombe Joseph Magufuli inafanya jitihada zote kujua kuhusu kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda.

Wazazi wa Azory Gwanda wameomba msaada wa serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iendelee kufuatilia kujua taarifa kamili juu ya suala la kupotea mwandishi huyo wa Mwananchi Media Corporation ili ieleweke kilichompata mwandishi huyo ili wazazi na familia ya Azory Gwanda wafahamu yaliyomkuta kama bado yupo hai au amefariki .

Source : CHADEMA MEDIA TV

Mama Samia rais wetu anayo nafasi kubwa ya kulitibu taifa hili.

Nchi ilikuwa imechezewa sana na bila sababu za msingi.
 
Kutoweka kwa huyu mwandishi kunatatanisha kwani hata haijulikani alikuwa akiandika au akitafuta taarifa juu ya kitu gani ambacho kingeweza kuwa ndiyo sababu ya kutoweka kwake.

Hivi huko Mwananchi nao hawajui alikuwa akishughulika na habari gani?

Je kwenye magazeti ni habari zipi alizokuwa anaziandika, ili tujaribu kuunganisha doti?.

Hii ni tofauti kabisa na kutoweka kwa Ben Saanane, ambaye habarizilizosababisha apotee zinajulikana wazi.
Alikuwa akifatilia unyama uliofanywa kibiti ikiwemo ukatili na mauaji ya wasio na hatia kwa kuhisiwa tu eti ni magaidi ikapelekea wengi kuumizwa japo sio wahusika.But haki za watu huwa hazipotei bure.
Killing haijawahi kuwa solution Tza sio Rwanda.
 
Yote ni sababu ya jiwe kuwa na uswahiba na PAKA akampa roho chafu
Hakika mkubwa ameliacha taifa katika hali ya mgawanyiko sana. Kiasi ambacho hata viongozi walioshika kijiti baada yake, wanakuwa na mzigo wa kurejesha tabasamu kwa Watanzania.
 
Hakika mkubwa ameliacha taifa katika hali ya mgawanyiko sana. Kiasi ambacho hata viongozi walioshika kijiti baada yake, wanakuwa na mzigo wa kurejesha tabasamu kwa Watanzania.
Dawa ni wote walioshiriki uovu ni lzm wavune sabaya tayari bashite,musiba na wasiojulikana wakae mkao wa kuliwa kuni ziko jikoni
 
Dawa ni wote walioshiriki uovu ni lzm wavune sabaya tayari bashite,musiba na wasiojulikana wakae mkao wa kuliwa kuni ziko jikoni
Ni kweli mkuu huo mnyororo wa hao watu ukifyekwa itakuwa vyema.
 
Hii picha popote ilipo ichomwe moto hapa ni roho ya

Ili kuliponya taifa
Ni kweli mkuu, uponyaji unahitajika ndani ya mioyo ya watu.
Kutowawajibisha hawa watesi watu wataendelea kuona ni mwendelezo wa utawala wa yule.
 
nilisoma mahali humu kuwa kuna mtu alikula ya chuma ya kichwa live kwenyee jumba jeupe . Ni nani huyo?
 
04 June 2021

Baada ya kauli za kupingana kati ya ile ya waziri Prof. Palamagamba Kabudi wa serikali ya Tanzania alipohojiwa na BBC Swahili na ya msemaji wa Mkuu serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda hapo mwezi November 2017. Msemaji wa serikali Dr. Hassan Abbas alisema serikali iliyokuwa chini ya hayati rais John Pombe Joseph Magufuli inafanya jitihada zote kujua kuhusu kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda.

Wazazi wa Azory Gwanda wameomba msaada wa serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iendelee kufuatilia kujua taarifa kamili juu ya suala la kupotea mwandishi huyo wa Mwananchi Media Corporation ili ieleweke kilichompata mwandishi huyo ili wazazi na familia ya Azory Gwanda wafahamu yaliyomkuta kama bado yupo hai au amefariki .

Source : CHADEMA MEDIA TV

Pombe alimuua Bwana Azory.
Pombe alifuga na kuteua majambazi na yakawa yanatumia silaha za moto tulizonunua kwa kodi za watanzania kuporea fedha kutoka kwetu sisi watanzania masikini kisha wanagawana.

Pombe alaaniwe! Maiti yake ife tena na tena!
Poleni sana wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
Pumzika kwa amani ndugu yetu mtanzania mwenzetu Azory Gwanda.
 
Iundwe tume maalum kuchunguza haya matukio yaliyoshika kasi enzi za jiwe
Mkuu nakubaliana nawe, kwamba Mh. Rais aunde Tume Maalum ya Maridhiano na Upatanishi kwa matukio yote ya unyanyasaji, mateso, ukiukwaji wa Sheria na ukiukwaji wa Haki za Binadamu katika kupindi cha 2015-2021, ili kuleta mwafaka na wananchi kulijea katika shughuli zao kama kawaida. Kusiwepo tena makundi ya kikanda, kikabila, kimkoa, Kidini, ubaguzi kwenye vyama vya siasa na hata Mtanganyika na Mzanzibar. Hayati N. Mandela aliwahi kufanya hivyo kule Afrika ya Kusini alifanikiwa sana.
 
Iundwe tume maalum kuchunguza haya matukio yaliyoshika kasi enzi za jiwe
Ingefaa iwe hivyo, lakini sioni utashi wa kufanya hivyo.

Na hata ingefanyika, hizi tume zinazoundwa naona ni kwa manufaa ya wanaoziunda; maana hadi sasa zilizoundwa taarifa za tume hizo zinabaki huko huko zilikoundiwa.
 
Alikuwa akichunguza na kuandika juu ya mauaji yaliyokuwa yakifanywa na Polisi huku Rufiji kwa kusingizio cha kuwatafuta watu waliokuwa wakiua viongozi na Polisi.

Taarifa zisizo rasmi, watu zaidi ya 80 waliuawa. Hiyo ilisemwa na wabunge Zito na Bwege Bungeni. Lakini wapo waliofanywa vilema, wengine majina yao yalisomwa Bungeni.

Azory alikuwa akifanya uchunguzi ambao ungeianika Serikali katika kuua raia wake.
Asante sana mkuu 'Bams' kwa taarifa hii iliyonipa mwanga zaidi kuliko nilivyowahi kuupata juu ya mwandishi huyu.

Kwa hiyo inaeleweka wazi sasa serikali ndiyo inayotakiwa kutoa jibu kuhusu upotevu wake.
 
Alikuwa akifatilia unyama uliofanywa kibiti ikiwemo ukatili na mauaji ya wasio na hatia kwa kuhisiwa tu eti ni magaidi ikapelekea wengi kuumizwa japo sio wahusika.But haki za watu huwa hazipotei bure.
Killing haijawahi kuwa solution Tza sio Rwanda.
Asante mkuu 'kalonji'.

Kwa hakika "killing" haiwezi kuwa utatuzi wa kila jambo. Ni njia ya mkato ya kuondoa tatizo kwa muda, bila ya kuliondoa kwa muda mrefu.
 
Mimi naamini vitu vingine sio JIWE alikuwa anatuma bana, wao walikuwa wanajipendekeza kwa kuua, kuteka ili kumfuraihisha....na kama ulivyo ada kila binadamu anapenda sifa, akawa anaridhia hayo mambo...sasa afanyeje?[emoji848]

Au nasema uwongo ndugu zangu??

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom