Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
shule ya mburahati hipo karibu na kituo kikubwa cha mburahatiBaadhi ya Wazazi na Walezi wenye Watoto katika Shule Msingi Mburahati wamefika shuleni hapo mchana wa leo Julai 22, 2024 kwa lengo la kuwafuata Watoto wao kutokana na hofu iliyotanda ikidaiwa kuna Watu wanania ya kuwateka
Inadaiwa kulitokea gari ain ya Noah nyeusi ambayo haina namba iliyokuwa karibu na maeneo ya Shule, hali hiyo ikawashtua baadhi ya watu na kuanza kupeana taarifa juu ya uwepo wa gari hiyo ambayo baada ya muda iliondoka
Baada ya taarifa hiyo kusambaa Wazazi na Walezi wakakusanyika eneo la shule wakitaka kujua kama watoto wao wapo salama, wakazuiwa getini.
Idadi ilipoongezeka uongozi wa Shule ukaita Jeshi la Polisi kusaidia kuwatuliza Wazazi na Walezi, ambapo wakaanza kuwatoa Watoto, wakatumia Spika kuita majina ya Watoto kisha Mzazi au Mlezi anaingia ndani anathitishwa kama ndiye mwenye Mtoto anamchukua na kuondoka.
Watoto ambao hawakuwa na watu waliokuja kuwachukua wakalazimika kubaki Shuleni kwa muda