Wazazi wajaa Shule ya Mburahati kuwachukua Watoto, hofu ya kutekwa baada ya Noah nyeusi kuonekana

Wazazi wajaa Shule ya Mburahati kuwachukua Watoto, hofu ya kutekwa baada ya Noah nyeusi kuonekana

Huo mda wote wanaitana wameshindwa kuita polisi ikaihoji hiyo noah isiyo na namba.
Jamani ukiwa na mtoto sasa hivi roho juu juu
 
tumuulize samia na IGP ni drama au movie za kiindi ccm
GTBlcJ7W0AA_Vrr.jpg
 
Baadhi ya Wazazi na Walezi wenye Watoto katika Shule Msingi Mburahati wamefika shuleni hapo mchana wa leo Julai 22, 2024 kwa lengo la kuwafuata Watoto wao kutokana na hofu iliyotanda ikidaiwa kuna Watu wanania ya kuwateka

Inadaiwa kulitokea gari ain ya Noah nyeusi ambayo haina namba iliyokuwa karibu na maeneo ya Shule, hali hiyo ikawashtua baadhi ya watu na kuanza kupeana taarifa juu ya uwepo wa gari hiyo ambayo baada ya muda iliondoka

Baada ya taarifa hiyo kusambaa Wazazi na Walezi wakakusanyika eneo la shule wakitaka kujua kama watoto wao wapo salama, wakazuiwa getini.

Idadi ilipoongezeka uongozi wa Shule ukaita Jeshi la Polisi kusaidia kuwatuliza Wazazi na Walezi, ambapo wakaanza kuwatoa Watoto, wakatumia Spika kuita majina ya Watoto kisha Mzazi au Mlezi anaingia ndani anathitishwa kama ndiye mwenye Mtoto anamchukua na kuondoka.

Watoto ambao hawakuwa na watu waliokuja kuwachukua wakalazimika kubaki Shuleni kwa muda
shule ya mburahati hipo karibu na kituo kikubwa cha mburahati
 
Haya mambo tunachukulia mzahamzaha kuna siku yatatokea maafa mahala ndio tutaanza kushikana uchawi, kuna hatari siku wananchi wakaua watu ndani ya noah nyeusi kwasababu tu mashaka.

Wenye noah nyeusi muishi Kwa tabadhari.
 
Ili swala limetapakaa kila kona wana nchii tupo loo juu kwa usalama wa watoto wetu uwongozi wa nchii upo kimya
 
Hizi drama, Gen Z wawili tu wa kenya walitosha kumaliza kila kitu.
Ona shule yenyewe utafikiri ya kabla ya uhuru!
 
Back
Top Bottom