Baada ya ajali ya moto uliochoma shule Kagera jana kuua watoto 10 na kujeruhi 7 wa kati ya miaka 6 - 10 [emoji853][emoji853] (May their little souls Rest in Heaven [emoji72][emoji72])
Naomba kuwauliza wanajamii wenzangu, je ni wakati gani kama mzazi/mlezi unaweza sema "It can't be helped. Mtoto NI LAZIMA aende boarding school."?
Ina maana tunakosa kabisa namna ya kuendelea kuishi na watoto wetu majumbani, chini ya uangalizi wetu wakaenda shule asubuhi na kurudi jioni kiasi cha kuwakimbiza boarding school wakiwa bado wadogo sana? Tukishawakimbiza boarding school katika umri huo mdogo, ni lini utapatikana muda wa kukaa nao na kuwajenga kihisia, kitabia na kiakili kama wazazi?
Hatuoni kama tunawapunja sana hawa watoto? Ama hata sisi wenyewe kwa kutoshiriki kikamilifu katika ukuaji wao?
[emoji2308][emoji2308][emoji2308][emoji2308]
Kiukweli vifo vya hao watoto viliniumiza sana, nilijikuta nina maswali mengi sana kichwani
Sijawahi kuwaza kuwapeleka wanangu boarding hata siku moja, pamoja na changamoto za wasaidizi wa kazi, wakati mwingine inafika wakati unakata tamaa kabisa lakini ni bora kusacrifice kazi yangu for the sake of the kids na sio kuwapeleka boarding
Kwa umri huo ni muda ambao watoto bado wanahitaji foundation kubwa sana kutoka kwa wazazi wote wawili, wanahitaji pia upendo na ukaribu na mzazi na pia inasaidia hata kujenga bond kati ya mzazi na mtoto
Ni umri ambao mtoto yupo katika stage ya kujifunza, kwa hiyo mengi anayojifunza anaangalia kutoka kwa walezi na hapa ndio mantiki ya wazazi inapokuja...naamini kila mzazi kuna namna ambayo anatamani amlee mtoto/watoto wake na kuna makuzi ambayo hatamani kumuona mtoto wake ameyapata especially baqdhi ya tabia ambazo baadae zinaweza kusababisha mtoto kuwa kiumbe wa hovyo, kwa hiyo umri huu ni wa kumtengeneza sana mtoto
Nawaza tu hao wanaokua boarding, wanajifunza mengi sana mazuri na mabaya, wanajifunza kutoka kwenye backgroubd za kila aina maaana kuna mchanganyiko wa watu wengi, sijui hata kama kuna ile upendo ambao angetakiwa kuupata kwa mzazi, wakati mwingine mtoto hata anapokua na jambo, sijui huwa anamweleza nani, either mwalimu au wanafunzi wengine?
Mimi nadhani serikali ingebadilisha tu huu utaratibu wa watoto wa shule za msingi kukaa boarding na sheria iwekwe ili wazazi waweze kuwajibika katika malezi ya watoto la sivyo tutatengeneza taifa lenye watu wa hovyo, irresponsible citizens kwa sababu wamekua katika mazingira ambayo wazazi wao hawakua respinsible kwenye malezi yao na hakujifunza kutoka kwao
Mzazi anapata kabisa usingizi mtoto wake wa miaka 4 yupo boarding, hujui amekula, ameoga, anajisikiaje, tena mama ameingia leba kabisaa