Wazazi/walezi tuna-fail wapi?

Wazazi/walezi tuna-fail wapi?

Baada ya ajali ya moto uliochoma shule Kagera jana kuua watoto 10 na kujeruhi 7 wa kati ya miaka 6 - 10 [emoji853][emoji853] (May their little souls Rest in Heaven [emoji72][emoji72])

Naomba kuwauliza wanajamii wenzangu, je ni wakati gani kama mzazi/mlezi unaweza sema "It can't be helped. Mtoto NI LAZIMA aende boarding school."?

Ina maana tunakosa kabisa namna ya kuendelea kuishi na watoto wetu majumbani, chini ya uangalizi wetu wakaenda shule asubuhi na kurudi jioni kiasi cha kuwakimbiza boarding school wakiwa bado wadogo sana? Tukishawakimbiza boarding school katika umri huo mdogo, ni lini utapatikana muda wa kukaa nao na kuwajenga kihisia, kitabia na kiakili kama wazazi? Hatuoni kama tunawapunja sana hawa watoto? Ama hata sisi wenyewe kwa kutoshiriki kikamilifu katika ukuaji wao?

[emoji2308][emoji2308][emoji2308][emoji2308]
aisee
 
Maisha yanaenda Kasi..majukumu yanazidi kuwa mengi..mahousegal hawaaminiki mzazi anaona Bora ampeleke mtoto boarding walau anahisi kutakuwa na usalama..ingawa kwa sasa usalama ni% chache Sana..kuzaa kwa mpango ni muhimu na suala la shule za boarding sidhani Kama linakwepeka kwa Life la sasa
 
Malezi ya usasa, kuiga, ubusy usiokuwa na kiasi nk hiv vinachangia kuharibu malezi. Wazazi wengi sasa wanais jukum lao nikuza na kutoa ela za matumizi tu kwa mtoto tumesahau misingi ya malezi bora
 
Ubusy usiokuwa na maana, zamani waliwezaje kulea watoto zaidi ya watano bila kuwapeleka boarding. Unakuta mtu ana mtoto mmoja na bado anampeleka shule za bweni ni ukichaa wa Hali ya juu.
 
Maisha yanaenda Kasi..majukumu yanazidi kuwa mengi..mahousegal hawaaminiki mzazi anaona Bora ampeleke mtoto boarding walau anahisi kutakuwa na usalama..ingawa kwa sasa usalama ni% chache Sana..kuzaa kwa mpango ni muhimu na suala la shule za boarding sidhani Kama linakwepeka kwa Life la sasa
Mkuu ubize gani huo wa kushindwa kulea mtoto mdogo? Kweli inasikitisha mtoto wa miaka 3-10 yupo boarding na wazazi wapo wanakula bata. Baadae akikosa upendo kwa wazazi tutamlaumu nani.
 
Mkuu ubize gani huo wa kushindwa kulea mtoto mdogo? Kweli inasikitisha mtoto wa miaka 3-10 yupo boarding na wazazi wapo wanakula bata. Baadae akikosa upendo kwa wazazi tutamlaumu nani.
Hao walaji Bata na wazimu wao..nimezungumzia wale wazazi waliotingwa Katika utafutaji ambao inawawia vigumu kubalance na malezi na kupeleka watoto shule za boarding..ingawa kwa mtoto wa miaka 3 Hadi 10 kumpeleka boarding si sawa .
 
Inasikitisha sana, wazazi wa kileo tunafeli sana. Haiwezekani mtoto mdogo anayehitaji upendo wa wazazi anapelekwa kulelewa na watu baki. Utamfundisha lini tabia, upendo nk.
 
Baada ya ajali ya moto uliochoma shule Kagera jana kuua watoto 10 na kujeruhi 7 wa kati ya miaka 6 - 10 [emoji853][emoji853] (May their little souls Rest in Heaven [emoji72][emoji72])

Naomba kuwauliza wanajamii wenzangu, je ni wakati gani kama mzazi/mlezi unaweza sema "It can't be helped. Mtoto NI LAZIMA aende boarding school."?

Ina maana tunakosa kabisa namna ya kuendelea kuishi na watoto wetu majumbani, chini ya uangalizi wetu wakaenda shule asubuhi na kurudi jioni kiasi cha kuwakimbiza boarding school wakiwa bado wadogo sana? Tukishawakimbiza boarding school katika umri huo mdogo, ni lini utapatikana muda wa kukaa nao na kuwajenga kihisia, kitabia na kiakili kama wazazi? Hatuoni kama tunawapunja sana hawa watoto? Ama hata sisi wenyewe kwa kutoshiriki kikamilifu katika ukuaji wao?

[emoji2308][emoji2308][emoji2308][emoji2308]
Tambua wazazi wengine wanaishi sehemu ambazo hakuna shule kwa nn ajali ikishatokea tunalaumu Sana kwa nini usije keta hii mada kabla .kaa kimya tena utulie kabisa
 
Maisha yanaenda Kasi..majukumu yanazidi kuwa mengi..mahousegal hawaaminiki mzazi anaona Bora ampeleke mtoto boarding walau anahisi kutakuwa na usalama..ingawa kwa sasa usalama ni% chache Sana..kuzaa kwa mpango ni muhimu na suala la shule za boarding sidhani Kama linakwepeka kwa Life la sasa
Mtu anawezaje kumuamini Mwalimu/Matron ambae yuko miles away kuliko dada wa kazi ambao yupo ndani ya nyumba?? Ina maana boarding ni salama zaidi kuliko nyumbani ambapo unaweza ukafuatilia mambo kwa ukaribu zaidi???
 
Mkuu ubize gani huo wa kushindwa kulea mtoto mdogo? Kweli inasikitisha mtoto wa miaka 3-10 yupo boarding na wazazi wapo wanakula bata. Baadae akikosa upendo kwa wazazi tutamlaumu nani.

Inafurahisha kweli tunapotaka kujifanya kuwa sie tuko busy kuliko watu wa mataifa mengine. 😄😄

Na nyumba nyingi unakuta zina baba na mama kabisa. Wanashindwa vipi kujiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha na u-busy wao bado wanampa mtoto muda na kumjali anakostahili???
 
Baada ya ajali ya moto uliochoma shule Kagera jana kuua watoto 10 na kujeruhi 7 wa kati ya miaka 6 - 10 [emoji853][emoji853] (May their little souls Rest in Heaven [emoji72][emoji72])

Naomba kuwauliza wanajamii wenzangu, je ni wakati gani kama mzazi/mlezi unaweza sema "It can't be helped. Mtoto NI LAZIMA aende boarding school."?

Ina maana tunakosa kabisa namna ya kuendelea kuishi na watoto wetu majumbani, chini ya uangalizi wetu wakaenda shule asubuhi na kurudi jioni kiasi cha kuwakimbiza boarding school wakiwa bado wadogo sana? Tukishawakimbiza boarding school katika umri huo mdogo, ni lini utapatikana muda wa kukaa nao na kuwajenga kihisia, kitabia na kiakili kama wazazi?

Hatuoni kama tunawapunja sana hawa watoto? Ama hata sisi wenyewe kwa kutoshiriki kikamilifu katika ukuaji wao?

[emoji2308][emoji2308][emoji2308][emoji2308]
Kiukweli vifo vya hao watoto viliniumiza sana, nilijikuta nina maswali mengi sana kichwani

Sijawahi kuwaza kuwapeleka wanangu boarding hata siku moja, pamoja na changamoto za wasaidizi wa kazi, wakati mwingine inafika wakati unakata tamaa kabisa lakini ni bora kusacrifice kazi yangu for the sake of the kids na sio kuwapeleka boarding

Kwa umri huo ni muda ambao watoto bado wanahitaji foundation kubwa sana kutoka kwa wazazi wote wawili, wanahitaji pia upendo na ukaribu na mzazi na pia inasaidia hata kujenga bond kati ya mzazi na mtoto

Ni umri ambao mtoto yupo katika stage ya kujifunza, kwa hiyo mengi anayojifunza anaangalia kutoka kwa walezi na hapa ndio mantiki ya wazazi inapokuja...naamini kila mzazi kuna namna ambayo anatamani amlee mtoto/watoto wake na kuna makuzi ambayo hatamani kumuona mtoto wake ameyapata especially baqdhi ya tabia ambazo baadae zinaweza kusababisha mtoto kuwa kiumbe wa hovyo, kwa hiyo umri huu ni wa kumtengeneza sana mtoto

Nawaza tu hao wanaokua boarding, wanajifunza mengi sana mazuri na mabaya, wanajifunza kutoka kwenye backgroubd za kila aina maaana kuna mchanganyiko wa watu wengi, sijui hata kama kuna ile upendo ambao angetakiwa kuupata kwa mzazi, wakati mwingine mtoto hata anapokua na jambo, sijui huwa anamweleza nani, either mwalimu au wanafunzi wengine?

Mimi nadhani serikali ingebadilisha tu huu utaratibu wa watoto wa shule za msingi kukaa boarding na sheria iwekwe ili wazazi waweze kuwajibika katika malezi ya watoto la sivyo tutatengeneza taifa lenye watu wa hovyo, irresponsible citizens kwa sababu wamekua katika mazingira ambayo wazazi wao hawakua respinsible kwenye malezi yao na hakujifunza kutoka kwao

Mzazi anapata kabisa usingizi mtoto wake wa miaka 4 yupo boarding, hujui amekula, ameoga, anajisikiaje, tena mama ameingia leba kabisaa
 
Very true [emoji53][emoji53]

Kuna umuhimu wa kuiga kuzaa kwa mipango kutoka kwa wenzetu wa Magharibi. Watu wawe wanaamua kuzaa wanapokuwa tayari kuwa responsible [emoji817][emoji817] badala ya watu kuzaa ili kuendeleza trend ama kufurahisha jamii na mwishowe kufelisha vizazi vijavyo.
Uzazi wa mpango kwa nchi yetu ni ngumu sana kwa sababu serikali haiungi mkono suala zima la uzazi wa mpango, mkuu wa nchi amekua busy akiwasisitiza watu kuzaa na kuwadescourage wale wanaoutumia njia za uzazi wa mpango kwa kigezo kwamba ni wanatumiwa na mabeberu

Wameshaambiwa matiti ya kunyonyesha wanayo, wanaume wapo, elimu bure, zaeni tu

Kwa msingi huu ni ngumu sana, wizara ya afya ilitakiwa kutoa elimu ya uzazi wa mpango nchi nzima ili kuwezesha kukabiliana na baadhi ya changamoto kama hizi

Kubwa zaidi, mzazi ambae an uwezo wa kumpeleka mtoto mtoto mdogo boarding that means anajiweza na ana elimu ya kutosha kuhusu uzazi wa mpango, ni kwamba tu hawataki kuwajibika kwa sababu ya huu utandawazi

Cha msingi ni kuweka sheria inayowabana wazazi kuwa responsible na malezi ya watoto wao, hizo ndio kazi za social workers hapa nchini, kufatilia mambo ya kijamii ila cha ajabu social workers wetu leo hii wanatembeza vyombo
 
Mamie Lizzy umeongea point kubwa sana

kikukweli kabisa na kiuhalisia faida za boaring ni chache sana kulinganisha na hasara zake

mara nyingi watoto wanaozoea kusomea boarding hasa wale wanaoanza mapema kabisa kusomea bweni huwa wanakosa deep connection na wazazi wao,inabaki tu ile ni baba na mama kwa sababu nimezaliwa nao ila ule upendo unaopaswa kutengenezwa kwa kuona ukuaji wa mtoto kuongea naye kujenga ukaribu naye huwa upo kidogo sana au haupo kabisa,nina ushahidi kadhaa juu ya hili

watoto waliozoea boarding ni wasiri kupindukia na hii ni kutokana na swala la kwamba wamezoea kujitegemea,hivyo mwanao anaweza akakabili matatizo mazito na kamwe usiwahi kujua wewe mzazi wake,akasolve kile kitu mwenyewe au akaingia kwenye shida nzito mnoo ukaje kujua wewe mzazi ni kuchelewa mnooo

lakini wapendwa raha ya family ikae pamoja mama baba na watoto wao,sasa mtoto miaka yote boarding anakaa kidogo kaanza kujitegema then anaenda kuoa/kuolewa utaenjoy lini na mtoto wako?

tuweni responsible wapendwa tuwalee watoto wetu wenyewe kuwe na sababu za msingi sana kuwapeleka watoto wetu wakalelewe huko na watu wengine ambao hawana lepe la uchungu,they have nothing to loose or to gain mwanao aharibikiwe au afanikiwe maishani.
 
Tukishawakimbiza boarding school katika umri huo mdogo, ni lini utapatikana muda wa kukaa nao na kuwajenga kihisia, kitabia na kiakili kama wazazi?

🙇‍♀️🙇‍♀️🙇‍♀️🙇‍♀️

Kwanza tuanzie hapo, sisi wazazi wenyewe wa siku hizi hizo akili tunazo? Wewe ukishaona mzazi anampeleka mtoto mchanga shule ya kulala, huna haja ya kuuliza, tayari unakua umeshajua tabia yake pamoja na kiwango chake cha akili kwa ujumla. Pengine kwa kiwango hicho cha akili, ni bora tu huyo mtoto akae huko boarding maana inawezekana akikaa nyumbani hali itakua mbaya zaidi.
 
Kwani mzazi akiwa busy anaondoka na nyumba??? Yani kazi za saa 8 - 17 ndo zisababishe watoto waondoke nyumbani up to 3 months at a time???

Mwingine unakuta mtoto kambwaga boarding school na yeye kajiwekea maid nyumbani. Like seriously.....?🤔🤔🤔🤔

Cha kuchekesha huyu huyu mzazi ukimkuta anakuambia "niko busy nawatafutia wanangu maisha" 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom