Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Mtoa mada unaonekana una msongo wa mawazo Hadi kushindwa kutoka nyumbani, punguza mawazo hizo Ni changamoto tu na mapito...

Member wengi watakupa mawazo mazuri Nini Cha kufanya.
Yeah, atoke hapo nyumbani, mtu kusema eti wewe sio mtoto Wangu sijui usije kwenye Kaburi langu, ni mikwara mbuzi sana hio, kama Mandonga tu, Kaburi ni Nini?

Wangapi Leo tunatembelea Makuburi ya Wapendwa wetu? Mbona wasabato wakishazika huwa hawarudi kutembelea WAFU?
 
Wazazi kama hawa ndio wanasababisha watoto wao wazekee nyumban imagin mzazi anasema mahari ndogo hakuna ndoa watakuja wengine hao wengine kashawatafuta? ujinga ujinga tu
Hahaha aisee yaani mtu akisoma hapa atafhani mtoa ushauri kashaolewa vile 🤣🤣🤣🤣
Kumbe mweee...anahangaika tuu
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida...
Mwambie jamaa akutoroshe akupangie sehemu ubebe mimba yake na ugome kabisa kurudi kwenu ikwezekana ubadilishe na namba zako za simu.

Baada ya muda wazazi wako watapata uchungu wa uzazi watakuja kukuomba msamaha na kurudisha mahusiano na wewe.
 
Nisome kwa makini nakujibu kwa mujibu wa sheria ya kiislaam...

Kwanza sheria ya kiislaam inatambua mpanga mahari ni muolewaji si mzazi wake. Yeye ndiye anayekubali au anayekataa...

Pili mzazi yeye hasa baba... Ni muozeshaji tu... Akikataa kuozesha kwa sababu zisizo za msingi za kisheria kama hiyo ya ujinga... Haki hiyo inadondoka... Inaenda kwa babu yako mzaa baba kama yupo... Kama hayupo inamfuata kaka yako baba mmoja mama mmoja... Kaka huyo hayupo... Anafuata kaka wa baba mmoja... Naye kama hataki... Haki inaangukia kwa baba mdogo au baba mkubwa... Na yeye kama hataki nenda kwa imam.

Na ndoa yako itafungwa... Mahari yako utaichukua wewe mwenyewe... Tumia mwenyewe kwa mapenzi yako ni yako sio ya wazazi au muozeshaji...

Na wala hizo laana zake hazifiki... Zaidi zitamrudia mwenyewe... Na vilevile anapata dhambi... Muombee tu msamaha kwa mola wako... Hajui alitendalo...
 
Mzee wetu wa ukoo (mchaga) alifukuza vijana kama wa 4 waliokuja na vi mahari vyao vya uchwara.

Binti yake alimsomesha Russia akahitimu udaktari bingwa wa kichwa (ubongo). Mzee wa ukoo alikua anataka mahari si chini ya mil 12 na zaidi.

Mmoja wapo akajifanya mwamba akampa ujauzito ili iwe nyepesi, mzee presha na sukari ikapanda. Baada ya kujifungua yule mtoto akaitwa jina la babu yake, kuanzia jina la mwanzo lakati na la mwisho yotee upande wetu.

Mwamba akaenda kufungua kesi, kesi (ikaendaa) sijui ikwaje mzee akashinda[emoji2]. Sasahizi binti yupo(wanaishi) denmkark na alishaolewa na mwanaume mwengine ambae ni (mshozi) ila dogo yupo (kabaki) kwa babu yake.

"Mzee alikua anasema alitumia pesa nyingi sana kumsomesha uko nje so hataki mahari ya ajabu ajabu"

"DADA kama unajiona una iyo thamani ya mil 10 basi tulia, watakuja tuu wenye uwo uwezo"
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida...
Beba mimba kubaliana kwanza na mwenzako.
 
Nyie ndio mnasababisha watu tunachachia majumban badae mnaanza makelele. Hyo 10M ukute mzee mwenyewe hata robo yake hana alafu anamvimbia kijana wa watu.
Acha ufalaaa wewe unajua gharama tunazotumia sie wazazi kuwalea nyie watoto? Msilete zenu bwana mtoto wa kike hatakiwa toka kwa bei nafuu. Ebo kwanza wanaume wenyewe wataenda kumtesa tuu mtoto na mihangaiko ya michepuko.

Mzee kashasema kuwa watakuja wengine, itakuwa alishajua kuna njemba anakuja kutoa hizo hela so mrembo atulie tuu. Daddy knows whats best for her
 
Wewe ni wale wale tu.
 
akienda akianza kuliwa kiboga mtamsaidia maana vitu vzuri gharama na yeye ashamuelewa msela wake
 
Mimi ngoja nikushauri direct, fanya liwezekanali huyo jamaa yako akupe mimba, then waamvie wazazi wako.una mimba yake tayari, then waambie mahali amekubali kulipa 3M ila kama kawaida ya mahali hailipwi yote, atalipa 70% tu na inayobaki itadaiwa polepole (wala hawataidai watasahau ukishaolewa)

Pia kaa chini na mama yako huyo ndio week point yako ya kuanzia, mueleweshe how life is, hao matajiri wengi wao walikua maskini tu kabla ila juhudi zao (sometimes wakishirikiana na wake zao waloanza nao maisha) ndio wakafikia hapo walipo, asitake mterezo wa kutaka uolewe na matajiri, mwambie wewe hujapata tajiri, kama wao wanataka uolewe na tajiri basi wakutaftie huyo tajiri akuoe. Pia muulize mama yako yeye alimkuta baba ako tajiri? atajiongeza.

Ila wazazi wako (hasa babako) ni mbulura kiukweli, yeye ndio alitakiwa ajue hali harisi kua maisha huanzia chini, ila yeye amekuona wewe kama ndio kitegauchumi chake, yani wanakuona kama ni mtaji wakuwakomboa[emoji34].
 
Back
Top Bottom