Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Siku hizi hali Ni Tete mtaani vyuma vimekaza kabisa hakuna michongo Wala nafasi za kutosha za ajira.
Vijana wengi wanahitimu vyuo wanarudi mtaani kutafuta ramani za maisha ila mambo hayaendi hawana CONNECTIONS kabisa.
Wengi wanakuwa ' liabilities' kwa wazazi wao licha ya kuwa na elimu ya juu.Utawakuta vijiweni kutwa nzima wanacheza bao mixer kubishana kwenye mambo ya Yanga na Simba.Inasikitisha Sana kuona vijana wetu wamekaa idol hawana lolote la maana wafanyalo.
Ni vibaya Sana kumuona mzazi anamshurutishwa mwanaye asepe nyumbani aende mjini kutafuta maisha.Je, ataendaje mjini wakati Hana connections Wala mchongo wa kueleweka.Wazazi wanatakiwa kuliangalia Hili suala kwa umakini Sana ili waweze kuwaokoa watoto kutoka kwenye Hali mbaya za kiuchumi.
Wazazi chukueni jukumu la kuwawezesha vijana wenu kiuchumi kwa kuwapa mitaji ya kuanzisha biashara ama kufanya kilimo kitakachowaingizia kipata wakati bado wanasikilizia michongo mingine.
Mwanao akishahitimu chuo tenga muda naye, mkae chini mzungumze umuulize Ni shughuli gani ambayo angependa kujihushisha nayo ya kumuingizia kipato.Akishakwambia Basi we mpe mtaji ama mfungulie hyo biashara aliyokupendekezea ili aweze kujiinua kiuchumi kuliko kukaa tu ku- idol mtaani.
Kwa mfano unaweza kumuwezesha mwanao kiuchumi kwa kumfungulia biashara ya duka la kuuza bidhaa mbali mbali, Banda la kuku, kupanda mimea Kama mboga na kadhalika. Naamini hi ndo njia pekee ambayo mzazi anaweza kumsaidia mwanaye baada ya kuhitimisha masomo.
Mwanao akiwa mwerevu Basi atajiongeza mwenyewe kwa kuikuza biashara uliyomuanzishia na kutengeneza faida kubwa.Na baada ya muda fulani atakuwa ameshapiga hatua kubwa ya kiuchumi na hakika wewe Kama mzazi utajivunia mwanao.