Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

Kwa hiyo utatakiwa ujenge nyumba ya kuishi wewe na mkeo na watoto ,Kisha baadaye watoto nao uwajengee nyumba waishi wao na wake zao


Something is not right 😃
 
Mzazi mkristo anatakiwa awe na mali za kusupport hadi wajukuu.

Umasikini ni tatizo
Lazima awepo wa kubreak chain ya umasikini, inawezekana wewe mtoto ndiye wa kubreak umasikini huo Ili uachie wanao Hadi wajukuu

Anza mkakati huo usibaki kulalamika tu
 
Hata mzazi pia hakujileta duniani, huyo mtoto kwa kuwa "ameshagundua hiyo mistari ya biblia" aanze yeye kuwatafutia mitaji wanae na wajukuu
Lakini hakuchagua kuja huku duniani.

Yeye ameletwa tu na watu wawili waliokua kwenye zoezi ya kutimiza “ haja zao za kimwili.

Ana haki ya kupewa japo ‘kianzio’.
 
Mabisho kibao kibantu walioachiwa urithi wametapanya wangine wameuza ili waende kwa madiba wengine wamelia bata urithi wa mtu mweusi ni elimu tu mpaka atakapojitambua
 
urithi upo dunia nzima
 
Yeah elimu katika Dunia ya saivi ni urithi mkubwa ...Kwa sababu elimu au maarifa ndio chanzo Cha utajili wote unao ujua ..
Ukitoka kuona umuhimu wa elimu nenda kijijini utakuta mtu ana ng'ombe 500 af anaishi kwenye nyumba ya nyasii na anamaisha magumuu akati ng'ombe mmoja anauzwa ad 2 million......
 
Uzi wako una mantiki iliyotukuka..jamani tuwaandalie watoto wetu kesho yao..
 
Wangapi wana elimu na wanatangatanga? Mpe mtoto mali aendeleze acheni uchoyo...jenga nyumba nyingi..wape wtt kila mmoja yake...aanzie hapo hata kuchukua kodi ili imsaidie mtaji...
 
Hivi kwa mfano unaacha urithi wa ulozi/uchawi aka teknolojia ya kiafrika si inakubalika wajameni au?
 
Wangapi wana elimu na wanatangatanga? Mpe mtoto mali aendeleze acheni uchoyo...jenga nyumba nyingi..wape wtt kila mmoja yake...aanzie hapo hata kuchukua kodi ili imsaidie mtaji...

Una akili sana. Wazazi wapumbavu ndio wanasema elimu ni urithi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…