Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

Huu uzi bora zaidi kwa 2024. Wazazi waache kujificha kwenye kichaka cha "elimu ni urithi"... mtoto anatakiwa arithishwe mali na vitega uchumi. Tuache longolongo ya kusema elimu ni urithi. Ubaya ni kwamba siku hizi watoto ndo wanawarithisha wazazi. Mtoto akishapata ajira anajitokeza mshenzi mmoja kwa jina la mzazi na kuanza kutaka mwanae amtunze ikiwemo kumjengea nyumba wakati yeye ndo alitakiwa kumpa nyumba mwanae.
Kwa hiyo utatakiwa ujenge nyumba ya kuishi wewe na mkeo na watoto ,Kisha baadaye watoto nao uwajengee nyumba waishi wao na wake zao


Something is not right 😃
 
Mzazi mkristo anatakiwa awe na mali za kusupport hadi wajukuu.

Umasikini ni tatizo
Lazima awepo wa kubreak chain ya umasikini, inawezekana wewe mtoto ndiye wa kubreak umasikini huo Ili uachie wanao Hadi wajukuu

Anza mkakati huo usibaki kulalamika tu
 
Hata mzazi pia hakujileta duniani, huyo mtoto kwa kuwa "ameshagundua hiyo mistari ya biblia" aanze yeye kuwatafutia mitaji wanae na wajukuu
Lakini hakuchagua kuja huku duniani.

Yeye ameletwa tu na watu wawili waliokua kwenye zoezi ya kutimiza “ haja zao za kimwili.

Ana haki ya kupewa japo ‘kianzio’.
 
View attachment 2897775


tunaanza na mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi​


Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na
Bwan
a”

NIMEGUNDUA WAZAZI WA ZAMANI WASIOENDA SHULE WANA AKILI KULIKO WAZAZI WA KISASA.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Elimu ni basic need kama kumpa mtoto chakula, Hivi unaweza wapa watoto chakula ati ndio useme Urithi,
Elimu ni basic need Kwa mtu inayomsaidia kutumia Rasilimali. Mzazi unapaswa uache Urithi WA rasilimali ambazo mtoto atazitumia kuendesha maisha yake baada ya kupewa elimu. Elimu bila Rasilimali ni Sawa na mdomo pasipo Meno.

Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila baada ya kumaliza tu chuo bado baba akaja kumpa urithi wa mali kijana wake yaani kampuni ya Mohammed Enterprises

Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.

Hujamrithisha mtoto Mali ataachaje kukosa Ajira?

Maisha ni yaleyale Ila binadamu ndio wanajifanya yaonekane yamebadilika


Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa mali ?
Mabisho kibao kibantu walioachiwa urithi wametapanya wangine wameuza ili waende kwa madiba wengine wamelia bata urithi wa mtu mweusi ni elimu tu mpaka atakapojitambua
 
mkuu toka miaka ya 1700s mpaka leo familia tajiri sweden ni Wallenberg family. utajiri wameupata kwa kurithisishana vizazi na vizazi vya hiyo familia. aliyetafuta mali Per Hansson Wallenberg alishakufa toka mwaka 1741 yaani miaka 300 iliyopita . ila mpaka leo vitukuu vyake ndio wanaendeleza utajiri huo
urithi upo dunia nzima
 
Mkuu MKATA KIU

Kwanza kabisa andiko hili ni zuri, ila huenda kuna kitu kidogo naona hakipo sawa.

Umezungumzia kipindi wazee wetu walikuwa wakiwaachia urithi watoto wao na kipindi cha sasahiv wazazi wetu wakitupa elimu.

Mosi, unaongelea vipindi tofauti hapa,kipindi hicho wazee wa wazee wetu hata elimu ilikuwa ni jambo gumu, hivyo mtoto anakuwa katika kusimamia mali za mzee wake.mfano kuchunga ngo’mbe na mashamba, kijana tangu akiwa mdogo mpaka anakuwa mkubwa anafundishwa ni namna gani ya kusimamia mali ya kwao.

Hivi sasa ni kipindi cha teknolojia tunapatiwa elimu mbadala wa yale yaliyofanyika miaka ile. Elimu ina upana wake, kuna watu wanasomea injinia, ufundi wa magari, majengo, udereva na vitu vingi.

Kama mtu yupo na ujuzi fulani kutokana na elimu tayari ni urithi huo.
Lakini mifumo mibovu ya elimu ya sasa inatengeneza “entitlements mentality” hasa kwa sisi vijana.

Tukitegemea kwamba tutapomaliza shule tutapata favor ya kuwa sehemu fulani sababu ya elimu yetu.

Huwezi kumfananisha kijana aliyeshinda home tangu mdogo akisimamia ngo’mbe na kukosa elimu na aliyeshinda darasani hajui hata ngo’mbe anachungwa vipi.

Elimu ni urithi.
Yeah elimu katika Dunia ya saivi ni urithi mkubwa ...Kwa sababu elimu au maarifa ndio chanzo Cha utajili wote unao ujua ..
Ukitoka kuona umuhimu wa elimu nenda kijijini utakuta mtu ana ng'ombe 500 af anaishi kwenye nyumba ya nyasii na anamaisha magumuu akati ng'ombe mmoja anauzwa ad 2 million......
 
Uzi wako una mantiki iliyotukuka..jamani tuwaandalie watoto wetu kesho yao..
 
Wangapi wana elimu na wanatangatanga? Mpe mtoto mali aendeleze acheni uchoyo...jenga nyumba nyingi..wape wtt kila mmoja yake...aanzie hapo hata kuchukua kodi ili imsaidie mtaji...
 
Hivi kwa mfano unaacha urithi wa ulozi/uchawi aka teknolojia ya kiafrika si inakubalika wajameni au?
 
Wangapi wana elimu na wanatangatanga? Mpe mtoto mali aendeleze acheni uchoyo...jenga nyumba nyingi..wape wtt kila mmoja yake...aanzie hapo hata kuchukua kodi ili imsaidie mtaji...

Una akili sana. Wazazi wapumbavu ndio wanasema elimu ni urithi
 
Back
Top Bottom