Wahaya, Wachagga, Wanyakyusa wanalima na kula ndizi. Ndizi ni tunda lenye maajabu yake, na moja ya maajabu ni kwamba huongeza uwezo wa kufikiri na uimara wa afya.
Makabila haya wengi ni wasomi na kujitambua Sana yaani akili nyingi.
Sasa basi, turudi kwenye mada ya kwamba Watanzania wengi wanapenda kuoa mwanamke wa aina gani?
Wanaume wengi na wasiowaelewa wanataka wapate mwanamke wa kuitikia 'ndiyo" kwa kila Jambo na pia huyo mwanamke aisiwe na rasilimali yeyote.
Sasa kwa muktadha huu, mtu anayetaka mwanamke atakwepa kuoa makabila ya aina hiyo kwa sababu hayo makabila ni nadra sana kumpata mwanamke kishoia aisiyejitambua.
Halafu, siku zote mchawi hawezi kumkubali MCHA MUNGU. Nimeandika kwa herufi kubwa ili kutia msisitizo.
Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa ni wacha MUNGU sana. Sasa Kama mtu ni mchawi yaani ni mtu wa Mambo ya Giza nene, hawezi kukubali mwanae aoe mcha Mungu kwa sababu ataleta ushindani wa kiroho nyumbani.
Hilo la kwamba Wachagga huenda kwao au Wamachame wanaua sidhani kama ni za msingi sana, maana mtu akitaka kuua anaua tu haijalishi kabila. Lakini pia, kama ingekuwa Wamachame wanaua, basi kanda ya Kaskazini ingeongoza kwa mauaji.
Kwa sasa kanda inayoongoza kwa mauaji ni Kanda ya Ziwa ambapo wengi huko ni Wasukuma na siyo Wachagga.
Hilo la Wachagga kwenda kwao siyo tatizo bali ni Jambo zuri la kuiga pia.
Na pia Kama mkeo anaenda kwao uchaggani, basi na wewe tafuta siku uende kwenu.