Wahaya, Wachagga, Wanyakyusa wanalima na kula ndizi. Ndizi ni tunda lenye maajabu yake, na moja ya maajabu ni kwamba huongeza uwezo wa kufikiri na uimara wa afya.
Makabila haya wengi ni wasomi na kujitambua Sana yaani akili nyingi.
Sasa basi, turudi kwenye mada ya kwamba Watanzania wengi wanapenda kuoa mwanamke wa aina gani?
Wanaume wengi na wasiowaelewa wanataka wapate mwanamke wa kuitikia 'ndiyo" kwa kila Jambo na pia huyo mwanamke aisiwe na rasilimali yeyote.
Sasa kwa muktadha huu, mtu anayetaka mwanamke atakwepa kuoa makabila ya aina hiyo kwa sababu hayo makabila ni nadra sana kumpata mwanamke kishoia aisiyejitambua.
Halafu, siku zote mchawi hawezi kumkubali MCHA MUNGU. Nimeandika kwa herufi kubwa ili kutia msisitizo.
Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa ni wacha MUNGU sana. Sasa Kama mtu ni mchawi yaani ni mtu wa Mambo ya Giza nene, hawezi kukubali mwanae aoe mcha Mungu kwa sababu ataleta ushindani wa kiroho nyumbani.
Hilo la kwamba Wachagga huenda kwao au Wamachame wanaua sidhani kama ni za msingi sana, maana mtu akitaka kuua anaua tu haijalishi kabila. Lakini pia, kama ingekuwa Wamachame wanaua, basi kanda ya Kaskazini ingeongoza kwa mauaji.
Kwa sasa kanda inayoongoza kwa mauaji ni Kanda ya Ziwa ambapo wengi huko ni Wasukuma na siyo Wachagga.
Hilo la Wachagga kwenda kwao siyo tatizo bali ni Jambo zuri la kuiga pia.
Na pia Kama mkeo anaenda kwao uchaggani, basi na wewe tafuta siku uende kwenu.
Km kila mmoja ataenda kwako kwa muda anaotaka kuna ndoa hapo?
Suala la ucha Mungu kwa maana ya dini kubwa mbili za kiislam na kikristo/kikristu ni mapokeo yaliokuja na yanaendelea kuongezeka kutokana na matengenezo ya kiimani yanavyo endelea.
Tabia za makabila yetu zinaandamana sana na malezi na mila na desturi na hivi vina uhusiano na mazingira yaliyo mzunguka mhusika tangu kutungwa kwa mimba mpaka kufikia umri wa ndoa.
Mila nyingi za kitanzania ziliaminisha au kufundisha kuwa mwanamke" hana dini wala kabila" si kwa sababu mbaya ila inawezekana ikawa mbaya kwa "nyakati hizi"
Nguvu ya wazaz na ndugu wa mwanamke ina nafasi kubwa kwenye kuboresha au kuharibu ndoa yako "kimya kimya"
Kuliko ile nguvu ya wazaz na ndugu wa kiume ambapo dalili za ndoa kutofika mbali huonekana mapema sana kwa kua mambo mengi hayajifichi au hufanyika kwa uwazi zaidi hivyo km ndoa inakufa inakufa kwa " mshindo mkuu "kwa kuwa dalili huonekana mapeema.
Sasa jiulize vita ni vita ila je vita vya chini chini na vya hadharani vipi vina umiza kichwa?
Anaweza akawa sio mnyaki au mchaga kwa kuzaliwa ila familia yake ikawa imeolowea bukoba au moshi au mbeya kwa miaka mia au sabini au hamsini je huyu unadhani atakuwaje?
Je mfumonwa utatuzi wa migogoro kwenye makabila yetu upoje...namaanisha " oganizesheni na menejimenti" hasa kwenye mambo ya kijamii na kiuchumi?
Mfumo wq maisha baina ya wewe muoaji na hao waolewaji...tafsiri ya maisha,ndoa ,furaha,upendo...histori ya familia yenu na makabila uliyo yataja je kuna ndoa zenye tabu ambazo zinatoka kwenye makabila yenu na yao?
Nafasi ya wazaz kwenye kulinda mawazo mali elimu na mifumo ya kiuchumi walio iandaa kwa ajili ya hayo makablia na hilo kabila lenu k. Haita match ndoa itatumia nguvu kuitunza.