Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Kunakitu sijaelewa hapa kisheria, je aliua au alisababisha kifo? mimi najua kuna kuua na kusababisha kifo, mfano unapomchoma mtu kisu kwa kujihami ili asikudhuru, hiyo ni kuu bila kukusudia, lakini unapo jaribu kujitetea ili usidhurike kisha ukamsukuma mtu akaanguka na kujigonga kisha baadae akafa hapo ni kusababisha kifo. Wanataaluma mliobobea hebu nisaidieni hili.

Kuua ni kufanya kitendo cha kutoa mtu uhai, na kitendo hiki hata mtu asipokufa bado unashtakiwa kwa kosa la kutaka kuua ( aijalishi kwa kukusuduia au kutokusudia)

Kusababisha kifo ni kufanya kitendo au jambo ambalo litasababisha mtu kudhurika kisha kufa, kwa hili bahati nzuri mtu asipokufa panakuwa hakuna kosa wala kesi.
 
Pamoja na hayo yote lakini lazima tukubali kuna doa kubwa limeingia kwa mahakama na kwa mawakili wa serikali....ambalo hadi leo nashindwa kuelewa kama yule wakili wa serikali aliye kuwepo jana kama anazo akili timamu kweli au alilewa rushwa aliyopewa...
Kitendo cha kukubali ushahidi wa kijinga wa mke wa Dr Slaa kwakweli ni aibu kubwa kwa mahakama....
Kwakweli sidhani kama hukumu itaaminika kabisa...
Lulu atapewa kifungo cha nje hakuna jipya..............
Sheria ya ushahidi ndo inaamua ushahidi gani ukubalike,na kukubalika kupokewa kwa ushahidi siyo kwamba ndo utaamua hukumu,unakubalika halafu unapimwa ndo unaungsnishwa na ushahidi mwingine ili kutoa hukumu.
 
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Kama kichwa cha habar kinavyojieleeza hapo

Yule ngul wa sheria kibatala amepanga kukata rufaa haraka na mapema ili kumuokoa mteja wake asipigwe mvua zisizo na idad na jaji lumanyika

Kibatala kayaongea hayo nje ya mahakama alipokuwa akizungumza na waandish wa habar kuhusu kes ya mteja wake

Kibatara kadai hakuna ushahid wa moja kwa moja ambao umemukuta lulu na hatia ya kuuwa sema wazee wa mahakama wametoa mamuz kwa mihemuko

LONDON BABY
Mbona wazee wamesema hakukusudia, wamuachie tu jamani
 
Adhabu ya kuua bila kukusudia

Kifungu cha 198 cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania): Mtu yeyote ambaye anatenda kosa la kuuwa bila kukusudia atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha. Hatahivyo, kuna mambo mawili ya kuyazingatia wakati wa hukumu. Mosi, Jaji Rumanyika hatalazimika kukubaliana na kufuata maoni ya Wazee wa Baraza. Pili, kama Jaji naye atamkuta Lulu na hatia adhabu yaweza kupunguzwa kadiri ya mazingira ya tukio na kadhalika.
Duuh m nlijua ukiua bila kukusudia wanakausha kumbe maisha tena duuh.wakipunguza 30 anatoka na 50 mzee
 
Hivi nn maana ya kuwa na "wakili nguli" kama huyo wakati mteja wako anahaha kujitetea mwenyewe mahakamani? Mtoto wa watu maskini hajui hata aseme nini
 
Hukumu nov 13 sherehe za uhuru dec 9. Lulu akiwa na bahati atachomoka nov 13 au akikwama basi atapata msamaha wa upendeleo dec 9 akishindwa hapo ndo basi tena atatumikia kifungo tu au rufaa itamuokoa
#justthinkingloud#
 
Aliekufaa kafaa...japoo wakili kaonekana kabisa anambeba lulu but no way wamuachie tu mtoto wa watuu japo sio fair kwa Mama Kanumba ilaa maisha lazima yaendelee
 
Narudia tena

Jaji halazimiki kufuata maoni ya accessor's of the court, hao wazee wa baraza ni maoni yao kwa jinsi wanavyoisikiliza kesi lakini Jaji ndiye final say anaangalia sheria na siyo busara kama hao wazee
 
Jaji Rumanyika ameshatoa hukumu? Naamini bado. Wazee wa baraza wanashauri tu (kwa jinsi ninavyojua). Nipo tayari kusahihishwa/kuelimishwa.
Ushahidi uliokubaliwa jana kutoka kwa mke wa Dr slaa ndio ulipigilia msumari kuwa ataachwa huru kwa vimasharti vidogo kwa muda fulani......
Ushahidi wa jana uliniacha hoi sana kiasi kwamba kila mtu ameona mazingira ya kuachiwa yanalazimishwa........hao wazee wa baraza hawatozingatiwa na judge kabisa kama alikubali ushahidi wa mke wa DR SLAA
 
Adhabu ya kuua bila kukusudia

Kifungu cha 198 cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania): Mtu yeyote ambaye anatenda kosa la kuuwa bila kukusudia atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha. Hatahivyo, kuna mambo mawili ya kuyazingatia wakati wa hukumu. Mosi, Jaji Rumanyika hatalazimika kukubaliana na kufuata maoni ya Wazee wa Baraza. Pili, kama Jaji naye atamkuta Lulu na hatia adhabu yaweza kupunguzwa kadiri ya mazingira ya tukio na kadhalika.
Mkuu Jaji Lumanyika alishamswalika Yule Mtoto kuwa wakati anaondoka eneo la Tukio na Motokari Je alikuwa ana leseni ya Udereva? Na kama alikuwa nayo aliipataje wakati sheria za Nchi haziruhusu kwa umri ule kuwa na Leseni.? Pia haka katoto kaliweza kuwa na Mahusiano ya kingono katika Umri Mdogo ule? Yaani haka katoto kafungwe tu... Halafu nilikaona jana Mahakamani yaani kanahitaji maombezi na lipini lake kwenye ulimi.. Ushauri kalikopewa na Mange hakaukufanyia kazi Katoto haka kafungwe ili kawe mfano kwa vitoto vingine vya kike... Unajua Kamiviharibu watoto wangapi kujiingiza kwenye mahusiano ya ngono wakiwa na umri mdogo kama hako katoto.... Yaani kupitia hako Katoto kamehahalarisha Ngono ni mchezo wa kawaida.. Kafungwe tu vile Mahakama Itaona inafaa ila kasihurumiwe kafungwe tu
 
Haujajibu swali toa mfano John au Juma alifungwa nje kwa manslaughter
Manslaughter hakuna kifungo cha nje.Unakuwa umeua,yaani kitendo ulifanya (actus reus) ila hukuwa na dhamira ya kuua(mens rea )haipo lkn umeua.Hukumu yake ni kifungo maisha sema utetezi unaweza kupunguza adhabu lakini haiwezi kuwa kifungo cha nje.
 
Hukumu nov 13 sherehe za uhuru dec 9. Lulu akiwa na bahati atachomoka nov 13 au akikwama basi atapata msamaha wa upendeleo dec 9 akishindwa hapo ndo basi tena atatumikia kifungo tu au rufaa itamuokoa
#justthinkingloud#
Sidhani kama msamaha ni kwa kila mfungwa.
 
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Kama kichwa cha habar kinavyojieleeza hapo

Yule ngul wa sheria kibatala amepanga kukata rufaa haraka na mapema ili kumuokoa mteja wake asipigwe mvua zisizo na idad na jaji lumanyika

Kibatala kayaongea hayo nje ya mahakama alipokuwa akizungumza na waandish wa habar kuhusu kes ya mteja wake

Kibatara kadai hakuna ushahid wa moja kwa moja ambao umemukuta lulu na hatia ya kuuwa sema wazee wa mahakama wametoa mamuz kwa mihemuko

LONDON BABY
Lulu aliiambia mahakama kuwa walikuwa wanakimbizana na Kanumba, tena kanumba alikuwa na taulo tu!
Akaulizwa taulo halikuanguka?
Akajibu halikuanguka!

Asingemkimbia ndio asingemuua bila kukusudia.
 
Back
Top Bottom