Kunakitu sijaelewa hapa kisheria, je aliua au alisababisha kifo? mimi najua kuna kuua na kusababisha kifo, mfano unapomchoma mtu kisu kwa kujihami ili asikudhuru, hiyo ni kuu bila kukusudia, lakini unapo jaribu kujitetea ili usidhurike kisha ukamsukuma mtu akaanguka na kujigonga kisha baadae akafa hapo ni kusababisha kifo. Wanataaluma mliobobea hebu nisaidieni hili.
Kuua ni kufanya kitendo cha kutoa mtu uhai, na kitendo hiki hata mtu asipokufa bado unashtakiwa kwa kosa la kutaka kuua ( aijalishi kwa kukusuduia au kutokusudia)
Kusababisha kifo ni kufanya kitendo au jambo ambalo litasababisha mtu kudhurika kisha kufa, kwa hili bahati nzuri mtu asipokufa panakuwa hakuna kosa wala kesi.