Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Scientific calculator mzee iko sawa kwa maana kikokotoo cha simu hakijafungua mabano kwanza. Bali kikokotoo cha kisayansi kimezingatia MAGAZIJUTO.
Duuuuh
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Aisee hii hesabu ni ya shule ya msingi darasa la saba B!

Nikimkumbuka mwalimu wangu kwa sheria ya MAGAZIJUTO jibu sahihi ni 9

Yani ni hivi:

6÷2(2+1)=

6÷2x(2+1)=

6÷2x3=

(6÷2)x3=

3x3=9

Ni ajabu sana kuona watu mnajifnaya mmefika hadi chuo kikuu alafu tunawashinda sisi tulioishia darasa la saba na kimalizia na QT.
 
Mangwin wanazingua, eti jibu ni 1 dah hakika inashangaza.
 
Sawa Bro..
Tumia hizo hesabu kulipa tozo kamili...
 
Narudia tena hesabu haifanywi kwa kuiangalia kwa macho hesabu inafanywa kwa vitendo.....ukifanya kwa macho jibu ni 1 ila uchukue pen na karatasi uchanganue jibu ni 9.... kama mtu class kwenu ulikuwaga wa mwisho mwisho tafadhari usiingilie hili jambo ni busara ukampigia kipanga wa darasani kwenu akusaidie tuseme ukweri(in the late magufuli voice), O level ulitaga hesabu, A level ulitaga au hukufanya hesabu sababu O level ulikuwa unataga, chuo ukaikimbia eti leo sababu hatukujui gafla umekuwa mtalaamuna wa hesabu 🤣 , daaah..una tofauti gan na lile jitu lililomwambia magu limepata gpa ya 7 ?....
 
Sawa mmepatia wote
madam hapana jibu ni 9 hesabu haina majibu mawili na ndio maana ni rahis kupata mia na ndio maana ma TO wengi wanatokaga PCM sababu haya msomo hayana janja janja majibu yake ni universal na vitu kama hivyo
 
Sioni tofauti ya MAGAZIJUTO na BODMAS
MA = BO
GA = D
ZI = M
JU = A
TO = S


BODMAS; B= Brakets, O=Order.(powers) etc. Lakini Katika Magazijuto hakuna order/exponent.

(BODMAS)=PEDMAS; P= paranthesis, E=Exponents etc.

Juu ya yote hazipishani sana.
 
VILAZA NI WENGI KWENYE HII NCHI, HESABU NI JANGA LA TAIFA

6/2(2+1)
6/2(3)

Ukifingua mabano inakua

6/6 = 1

Hawa fedhuli wanaosema ukifanya kilicho ndani ya mabano unakua umefungua mabano walisoma hesabu shule za Kata.
 
VILAZA NI WENGI KWENYE HII NCHI, HESABU NI JANGA LA TAIFA

6/2(2+1)
6/2(3)

Ukifingua mabano inakua

6/6 = 1

Hawa fedhuli wanaosema ukifanya kilicho ndani ya mabano unakua umefungua mabano walisoma hesabu shule za Kata.
Wewe umeeleza vizuri kwa ufupi na kwa usahihi.
Jibu ni 1
 
VILAZA NI WENGI KWENYE HII NCHI, HESABU NI JANGA LA TAIFA

6/2(2+1)
6/2(3)

Ukifingua mabano inakua

6/6 = 1

Hawa fedhuli wanaosema ukifanya kilicho ndani ya mabano unakua umefungua mabano walisoma hesabu shule za Kata.


Maana ya mabano ni ufanye kwanza kilichomo ndani ya mabano na sio ufungue mabano, kuna tofauti kati ya kufungua mabano na kufanya kilichomo ndani ya mabano ingawa katika math expression fulani majibu yanaweza kuwa sawa lakini sio kwa expression zote hususan zile zinazojumuisha operations za jumlisha na toa.

Mfano katika expression hii 2(3+4), ukifanya kilichomo ndani ya mabano unapata; 2×7=14, na ukifungua mabano kwa njia ya (association??) itakuwa 2(3+4) inakuwa 2×3+2×4, hii ni sawa na [(2×3)+(2×4)]=14, hivyo kwa case hiyo utaona ukifanya kilichomo ndani ya mabano au ukafungua mabano unapata majibu sawa.

Hivyo "Ma" katika Magazijuto inataka uanze kufanya, kukokotoa au kurahisisha kwanza kile kilichomo ndani ya Mabano kwa expressions zinazo involve operations za kujumlisha na kutoa na sio "kufungua mabano".

Umetumia neno baya sana kuita watu "fedhuli", tukikuripoti unakula ban.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…