ndo maana hesabu zikaandikwa kwa namba na sio maneno, wewe kaa na jibu lako na mimi nikae na langu, Na ndo maana scientific calculator original (ambayo siyo fake) itakuletea jibu 1 kwakua ile imeundwa kwaajili ya calculation kwaiyo inakwepa makosa yote ya kimahesabu. ila calculator ya simu ile ni ziada tu inaweza ikaleta majibu tofauti kwakua sio kazi ya simu kufanya calculation.
Kwa ninavyokuona hatuwezi kufikia huu maelewano kwenye huu mjadala ni sawa na 6 mkiwa wawili pande tofauti kuna atakayeona ni tisa na mweingine ni sita. kwaiyo huenda wote tupo sahihi kutokana na upande tuliokaa.
Uko mweupe sana kwenye mathematics, kila kauli unayo itoa inaonenya ni jinsi gani kwenye huu ukurasa haujui au umekariri kupindukia.
ndo maana hesabu zikaandikwa kwa namba na sio maneno,
Yes nikisea unakariri sijakosea. Number ni symbol of communication kama zilivyo herufi. Wakati wengine wana 1 hadi 9 warumi nao wanazo za muundo wao na waarabu vivyo hivyo.
Sentensi kama "Tulikuwa watu saba kati yetu wanawake wawili wanaume watano" katika number inawezwa kuandikwa hivi 7 = 2 + 5. Ya kwanza ndio tunaita words expression na ya pili tunaita numerical expression zote zina convey the same meaning.
1 hadi 9 na A hadi Z ni alama za mawasiliano na zinapatikana popote kwenye aina yoyote ya taaluma. Matendo kama kupunguza (kutoa), kuongeza (kujumlisha) ndio yanayoleta neno hesabu.
In words expression "Juma alimpa Jesca kalamu nane kati ya 20 alizokuwa nazo, aliongeza kalamu zingine kumi na tano kabla hajazigawa kwa kila mmoja kwenye familia ya watu tisa kwa usawa hivo hivo kila mmoja alipata kalamu 3"... in numerical expression inakuwa
[{(20-8)+15}÷9] = 3.
One mistake tu kwenye numerical expression either kwa wrong placement ya mabano inabadili maana totally. Mfano kwa hapo juu numerical expression kama hii
[(20-8)+15÷9] haileti 3 ambayo ni jibu la maana iliyokusudiwa mwanzo ingawa number zilizotumika ni zile zile na operational symbol ni zile zile zinazohitajika kasoro brackets husika hazipo...
Lengo la kubadili Words to numerical au numerical back to words expression ni kutest validity ya maana iliyokusudiwa kama haijabadilika ili kupata usahihi wa kinachotafutwa.
Kila numerical equation ina majibu ila si kila jibu lina reflect maana iliyokusudiwa. Na hiyo ndio hesabu sasa. Sio mikunjo ya 123 hadi 10.
So tusipeane mzigo wa kuanza kufundishana hesabu ni nini. Ukitaka kujua zaidi mwanao kwanini mwalim wake wa hesabu anamwambia ahesabu number kisha aziandike kwa maneno.
Na ndo maana scientific calculator original (ambayo siyo fake) itakuletea jibu 1 kwakua ile imeundwa kwaajili ya calculation kwaiyo inakwepa makosa yote ya kimahesabu
Again tena hii inaonesha hata neno Calculator hulijui maana ake.
Calculator/Kikotoo ni kifaa kinacho-perfom calculation/ukokotoaji under specific instructions. Vikokokotozi kama hicho unachodai kua ni Og sio fake kile ni programmable device ambacho kina perfom calculation under specific instructions.
All modern calculators hazitumii standard hiyo iliyo kuepo enzi hizo za 1917 that a÷b(c) ni sawa a/(b×c).
Kitendo cha kusema imeundwa maana ake unatakiwa uelewe iko programmed. Kua programmed ni kupewa set of instructions za ku'execute kwa kila command inayotolewa.
So when rules changed basi na outcome inabadilishwa kwa mfano lel say kule value of pie ilikuwa 20/7 (hii value ya mfano tu) but now ni 22/7. For the same calculation itakupa majibu tofauti kwasababu zinapokea command na ku'execute taarifa kwa instructions tofauti.
calculator ya simu ile ni ziada tu inaweza ikaleta majibu tofauti kwakua sio kazi ya simu kufanya calculation.
Sentensi kama hizi ndio zinaonesha hata kile unacho kizungumza hukijui. Tuacheni ubishi badala yake tukae chini tujifunze tuelewe.
Leo ukichukua vipimo vya uingereza ukaenda kuvi-apply US vinakuingiza chaka kwasababu wanatumia standard tofauti. Hapo juu nilitoa mfano wa Gallon kwa Litre.
Ukichukua Calculator ambayo iko programmed kwa standard za UK ambapo 1 Gallon kwa 4.546Litre ukaitumie US ambapo standard zao ni 1 Gallon kwa 3.872Litre itakuaje?
Utaiita fake au?
TUJIFUNZE KUELEWA.
Huku kukariri kwetu bila uelewa ndio unaofanya tukitoka nje ya mipaka yetu tunakuwa USELESS.