Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Taabu kwelikweli,

Hivi mtu akiandika 2a sio sawa na 2×a ??!!, kama ni sawa sasa utapingaje kwamba 2(2+1) sio sawa na 2×(2+1) ??!!, kumbuka katika Magazijuto "Ma" inakutaka ukokotoe kwanza kilichomo ndani ya mabano na sio kuingiza kitu ndani ya mabano kutoka nje kwani ndani ya mabano kuna Operator (+sign) inayojitosheleza kufanya operation ya + within the brackets.

Hivyo:-
6÷2(2+1)=6÷2×(2+1)=6÷2×3=(6÷2)×2=9. Hapa ni sheria ya Magazijuto ndiyo inayofanya kazi.
Mkuu,

Umejitahidi sana kuwaelewesha ila hawataki tu basi!

Hawa jamaa ngumbaru kweli kweli
 
Duh...

Nimefatilia kuanzia post ya kwanza hadi hapa kuna kitu nimek'note. Most of you hapa tumekariri hesabu hatukuelewa hesabu.

Hii expression ya 6÷2(2+1) ukifata sheria ya bodmas jibu ni 9 sio 1.

Expression yenye kukupa jibu la 1 ilipaswa iwe hivi 6÷[2 (2+1)] ama 6/[2 (2+1)] yani kwamba 6 iwe numerator na expression iliyobaki iwe denominator as parts of fraction.

Nasema tumekariri kwasababu hata aliyetoa real meaning ya BODMAS ni mmoja tu wengine wametoa definition ya kukariri.

BODMAS ni acronym ya Bracket Orders Divide Multiply Addition kisha Subtraction. Katika neno BODMAS hiyo O haijasimama kwa ajili ya neno Open Brackets, kitendo cha kusema hivyo ni wazi mtu hesabu amekariri. HAJUI, bahati mbaya wa mtu wa namna hii ndio mbishi na mjuaji kupindukia.

Kwa mfano kwenye expression kama hii, ni mda upi utadeal na hizo exponent au radical kwa kufata sheria ya BODMAS? 2²(4+3√9)-1.

So hapo kwa wenzetu tuliokariri hesabu, ile O katika neno BODMAS ni Orders sio Open Bracket tulio karirishwa darasani. Na baada ya kudeal na expression iliyo ndani ya braketi hupaswi kuzidisha au kugawanya hadi uhakikishe hakuna orders (radical ama exponents) kwenye expression yako. Then unafata kugawanya then kuzidisha kisha kujumlisha unamaliza na kutoa.

Hii expression imekua kama mtu unamwambia atofautishe kati ya 10,001 na 11,000. Hizo number zikitamkwa kimazoea unaweza fikiri ni number ile ile kumbe laa. Ila zikitamkwa kwa usahihi ndio utanote tofauti yake.

Mtu akisema "elfu kumi na moja 🤣🤣" utajua ni ipi kati ya hizo 2? Ni ngumu ila zikitamkwa kwa usahihi kwamba "kumi elfu na moja kisha kumi na moja elfu" respectively utajua ipi ni ipi ukiweka expression katika number.

Hapo pia tunafaa kuelewa tunapaswa kujua kwamba just a symbol tu inatosha kubadili maana katika expression ya hesabu.

Expression ya 6÷2(2×1) na 6÷[2(2×1)] ziko tofauti kabisa. Ya kwanza inakupa jibu 9 na ya pili jibu 1 kikanuni. Na tukitaka kuziona tofauti zake tuzibadili hizi expression katika maneno (sentence) kutoka kwenye symbol (number).

Expression "Mia tano na Moja" ikikosa neno "na" ikawa "Mia tano moja" ishabadili maana. In mathematics kukosea expression ni kukosea majibh mazima.

Kule juu tumeona Sci. Calculator imekokotoa as if ina deal na fraction part ambapo ile 6 kama numerator na the rest kama denominator.

Anyway nothing serious hapo ni issue ya programming, all modern scientific calculator inaleta jibu la 9.

Mwisho nashauri mambo machache tu.
1. Tuwe open kujifunza badala ya kubishana na hasira za kindezi kisa waona 9 mwingine anaona 6, tukubaliane tu perspective matters.

2. Vikokotoo viko programmed na binadam kama mie na wewe. Leo umejumlisha 3 na 4 kwenye kikotoo imekuletea 10 wakati ukihesabu vidole inakupa 7. Haina maana kua hauko sawa kwamba calculator always iko perfect.

Vikokokotoo ni visaidizi na vinatoa majibu kulingana na namna vilivyo programmed. Wrong expression will always yield wrong answers n.k kulingana na namna Calculator husika ilivyo.

Mfano calculator yenye function ya a×(b+c) kua ni sawa na (a×b)+(a×c) huwezi kuweka a×(b+c) ukiwa na intention ya (a×b)+c utegemee utapata jibu ulilokusudia. Kila symbol ina maana ake kwenye hesabu according to standard za eneo husika.

Leo 1.000 tz itaitwa ni 1 point Zero zero zero ilhali kwa standard za eneo jingine 1.000 ni 1 thousand symbol (.) Ikitumika kama thousands separator.

Mfano mwingine hizi expression zote zina maana moja na ziko sawa kwa standard tofauti katika maeneo tofauti duniani.

Kwa kutumia nafasi na alama ( , ) as decimal
200 000 789,05

Kwa kuacha nafasi wa kila thousands na kutumia alama ( . ) kwenye decimal
200 000 989.05

Hapa ( , ) kwenye kutenganisha maelfu na ( . ) kwenye desimali
200,000,989.05

Vile vile pia ( . )katika kutenganisha maelfu na ( , ) katika desimali.
200.000.989,05

Natoa maelezo meeeeeeeengi yanachosha ila lengo haswa ni kua tusikariri, tujifunze kuelewa.

1 Gallon ni sawa na 4.546 Litre
1 US Gallon ni sawa na 3.785 Litre
1 Imperial Gallon ni sawa na 4.546 Litre

Ya kwanza kama ya UK ndio inatumika hapa tz, sasa mfano mtu katumia kafanya conversion ndogo tu kama hiyo huyu kafanya kwa US Gallon na huyu kafanya kwa Imperial Gallon halafu wanabishana kila mtu anadai yuko sahihi anamuona mwingine kilaza kwasababu jibu lake liko tofauti na la mwenzie.

TUJIFUNZE KUELEWA WAJOMBA.
 
Taabu kwelikweli,

Hivi mtu akiandika 2a sio sawa na 2×a ??!!, kama ni sawa sasa utapingaje kwamba 2(2+1) sio sawa na 2×(2+1) ??!!, kumbuka katika Magazijuto "Ma" inakutaka ukokotoe kwanza kilichomo ndani ya mabano na sio kuingiza kitu ndani ya mabano kutoka nje kwani ndani ya mabano kuna Operator (+sign) inayojitosheleza kufanya operation ya + within the brackets.

Hivyo:-
6÷2(2+1)=6÷2×(2+1)=6÷2×3=(6÷2)×2=9. Hapa ni sheria ya Magazijuto ndiyo inayofanya kazi.
hiki 6÷2(2+1) na hiki ni vitu viwili tofauti 6÷2×(2+1) kwamba onaona hiyo isiyo na alama ya zidisha huyo mtu alipata uvivu wwa kuiandika sio.

Ukiona hivi 2(2+1) ni sawa na uambiwe kuna makundi mawili ya watu lakini katika hayo makundi mawili kuna wanaume wawili na mwanamke mmoja kila kundi, kwaiyo badala ya mtu kuandika hivi ((2+1)+(2+1)) akarahisisha kwa kuandika 2(2+1).

Kwa kupitia mfano huu ni sawa uulizwe una machungwa 6 alafu unatakiwa uwagawie hao watu walioko kwenye hayo makundi mawili je kila mmoja atapata machungwa mangapi bila kujali kama ni mwanamke au ni mwanaume?

Utakachotakiwa kufanya ni kujua kwanza idadi ya watu kwaiyo utajiuliza kama kuna makundi mawili ya watu ambapo kila kundi lina wanaume 2 na mwanamke 1 je jumla wote watakua wangapi? Utapata ni sita baada ya hapo utachukua idadi ya machungwa uliyonayo utagawanya kwa hao watu sita ambapo kila mmoja atapata chungwa moja.

jibu litakuja 9 endapo utachukua hayo machungwa ugawanye kwa idadi ya makundi ambapo ni 2 upate 3 alafu uje uzidishe na idadi ya watu waliopo kila kundi ambapo ni 3 kila kundi utapata 9 kitu ambacho ni impossible kwa akili za kawaida.

Kifupi tu ukiona hivi 2(2+1) ujue hiyo 2 ya nje inawakilisha kwamba kuna makundi mawili ya hivyo vitu vya ndani, kwamba kuna makundi mawili ya (2+1), kwaiyo huwezi ukafanya ulivyofanya wewe, utajiona upo sahihi kutokana na akili zako ila kiuhalisia ni kosa kubwa sana ilipaswa ujue kwanza jumla ya idadi ya vitu vilivyomo kwenye makundi yote mawili kwanza kisha uendelee na tendo lingine.

Nawasilisha kwako, kama hujaelewa hapa tena basi unahitaji maombi.
 
Unatakiwa ujue kutengeneza mathematical expression kutokana na swali husika
Kwa mfano wako wa machungwa ni hii 6÷(2(2+1))
 
Kama nje ya bracket hakuna tendo basi hakuna haja ya kweka mabano mengine

Ukishawekewa hivi 2(2+1) jua hicho ni kitu kimoja, wakati wa kufungua mabano lazima hiyo mbili ya nje iingie ndani ya hayo mabano ndio ufungue mabano, huwezi ukafungua mabano bila kuihusisha hiyo mbili ya nje.
 
Unahisi mwenzio anahitaji maombi but inshort wewe hapo ndio unahitaji maombi.

Jifunze kuelewa kwanza.

Tunapenda kujiakilify kuliko kujielimisha, Hii ndio shida yetu waswahili. Uliyo andika hapo ni mtazamo wako sio sheria za number.

Katika hesabu kitu chochote kisichobadili maana ni sawa sawa.

2 + 2 ni sawa na 3 + 1. Haijalishi hizo 2 au 3 au 1 ni machungwa au mahindi au binadam. Kwenye hesabu tunaongelea value.

Tunasema 2×(3-2) ni sawa na (2×3) - (2×2) ambayo ni moja kwasababu value yake haibadiliki.

Maelezo yako pia yaonesha namna ulivyo mchovu wa hesabu hasa kwenye symbol.

Hujiulizi kwanini kunapokua na number jiran ya bracket kama hakuna alama baina tunajua ni kuzidisha. Kwanini isiwe kutoa kujumlisha au kugawanya iwe kuzidisha tu?

Kama kweli zinakutosha akilini, unakataa 2(2+1) sio sawa na 2×(2+1) yet unafanya kuzidisha, kwanini usitoe au ujumlishe kama zina maana 2 tofauti?

Rudi Class ukajifunze tena kuhusu operational symbol. Hii 2(4) ni 8 sio 24 😂. Umejua ni 8 kwasababu kila penye number kisha bracket bila symbol basi kati kuna alama ya kuzidisha hivyo 2(4) ni sawa na 2×4.

Tena kwa maelezo yako ya hapo mwisho inaonekana hata maana ya haya matendo (Kujumlisha, kuzidisha, kutoa ama kujumlisha maana zake zinakupiga chenga).

Kwenye BODMAS hapo mnajichanganya kitu kimoja tu. Mjue Kuna tofauti kati ya kufungua mlango na kufungua mlango kisha kuingia ndani ama kutoka nje. Kitendo cha kufungua mlango kisha kuingia ndani umefanya vitendo viwili kwa mkupuo 😂.

Taratibu za kukoga anza na chota maji kisha jimwagie kichwani. Usianze kujimwagia miguuni kisa beseni lipo karibu na miguu. Utakuwa wrong.

Kitendo cha kumaliza operations zilizopo ndani ya jedwali ndio kufungua jedwali kwenyewe ambapo kinachobaki ni operational symbol zingine ambazo unatakiwa kurejea kwenye protocol uzitimize.

Mko weupe kwenye hesabu halafu mnajikuta mnajua kinoma noma 😂😂😂

Ila leo umetoa mpya mazee, kwamba 2 +3 = 5 lakini 5 hii sio sawa na 5 ya 4 + 1. What a genius duh 😂 kwamba 2(2+1) sio sawa na 2×(2+1) na we utakuta ni mwalim wa hesaby shule X unatuandalia wahasibu wa miaka ijayo.

Baadae tunapata wataalam kama Waziri flani tunaanza kutafuta mchawi 😂😂😂
 
nitabaki kusimamia kwamba 2(2+1) sio sawa na 2×(2+1) kwenye hii ya pili hiyo alama ya zidisha imeshatenganisha hiyo mbili
😂😂😂

Au sio... Dah em peleka hizo expression katika sentensi. I mean zitoe katika numerical expression uziweke katika words expression. 2 (2+1) na 2 × (2+1).

Ama ziandike in expansin form hizo expression zote 2. Ya kwanza na ya pili kisha utuoneshe utofauti wake. Unaijua hesabu kweli wewe?

Na pili kama haziko sawa kwanini umezidisha? Mkichwa uko sawa kweli mwamba?
 
hiki 6÷2(2+1) na hiki ni vitu viwili tofauti 6÷2×(2+1) kwamba onaona hiyo isiyo na alama ya zidisha huyo mtu alipata uvivu wwa kuiandika sio.

Ukiona hivi 2(2+1) ni sawa na uambiwe kuna makundi mawili ya watu lakini katika hayo makundi mawili kuna wanaume wawili na mwanamke mmoja kila kundi, kwaiyo badala ya mtu kuandika hivi ((2+1)+(2+1)) akarahisisha kwa kuandika 2(2+1).

Kwa kupitia mfano huu ni sawa uulizwe una machungwa 6 alafu unatakiwa uwagawie hao watu walioko kwenye hayo makundi mawili je kila mmoja atapata machungwa mangapi bila kujali kama ni mwanamke au ni mwanaume?

Utakachotakiwa kufanya ni kujua kwanza idadi ya watu kwaiyo utajiuliza kama kuna makundi mawili ya watu ambapo kila kundi lina wanaume 2 na mwanamke 1 je jumla wote watakua wangapi? Utapata ni sita baada ya hapo utachukua idadi ya machungwa uliyonayo utagawanya kwa hao watu sita ambapo kila mmoja atapata chungwa moja.

jibu litakuja 9 endapo utachukua hayo machungwa ugawanye kwa idadi ya makundi ambapo ni 2 upate 3 alafu uje uzidishe na idadi ya watu waliopo kila kundi ambapo ni 3 kila kundi utapata 9 kitu ambacho ni impossible kwa akili za kawaida.

Kifupi tu ukiona hivi 2(2+1) ujue hiyo 2 ya nje inawakilisha kwamba kuna makundi mawili ya hivyo vitu vya ndani, kwamba kuna makundi mawili ya (2+1), kwaiyo huwezi ukafanya ulivyofanya wewe, utajiona upo sahihi kutokana na akili zako ila kiuhalisia ni kosa kubwa sana ilipaswa ujue kwanza jumla ya idadi ya vitu vilivyomo kwenye makundi yote mawili kwanza kisha uendelee na tendo lingine.

Nawasilisha kwako, kama hujaelewa hapa tena basi unahitaji maombi.

Wewe ndiye unayehitaji maombi.

Unayo machungwa sita na unataka uyawagawie makundi mawili ya idadi ya watu waliomo waliomo ndani ya mabano je kila mtu atapata machungwa mangapi??

1---- Machungwa 6,
2----Idadi ya makundi 2.
3---Idadi ya Watu katika kila kundi ( 2+1)=3.
4--- Jumla ya watu 6.
5---kila mtu atapata machungwa mangapi??, idadi ya machungwa÷ idadi ya watu = kila mmoja atapata chungwa moja.

Mathematical representation ya jambo hilo ni hii hapa:-

6÷[2(2+1)]=1. na sio 6÷2(2+1).
 
😂😂😂

Au sio... Dah em peleka hizo expression katika sentensi. I mean zitoe katika numerical expression uziweke katika words expression. 2 (2+1) na 2 × (2+1).

Ama ziandike in expansin form hizo expression zote 2. Ya kwanza na ya pili kisha utuoneshe utofauti wake. Unaijua hesabu kweli wewe?

Na pili kama haziko sawa kwanini umezidisha? Mkichwa uko sawa kweli mwamba?
Hii 2(2+1) ni sawa na kusema (2+1)+(2+1) imerahisishwa tu
Lakini 2×(2+1) inabaki kama ilivyo, Japo vyote vitaleta jibu sawa
 
Wewe ndiye unayehitaji maombi.

Unayo machungwa sita na unataka uyawagawie makundi mawili ya idadi ya watu waliomo waliomo ndani ya mabano je kila mtu atapata machungwa mangapi??

1---- Machungwa 6,
2----Idadi ya makundi 2.
3---Idadi ya Watu katika kila kundi ( 2+1)=3.
4--- Jumla ya watu 6.
5---kila mtu atapata machungwa mangapi??, idadi ya machungwa÷ idadi ya watu = kila mmoja atapata chungwa moja.

Mathematical representation ya jambo hilo ni hii hapa:-

6÷[2(2+1)]=1. na sio 6÷2(2+1).
Kwa ufupi tu ukikutana na kitu cha namna hii x(ax+y) hiki ni kitu kimoja huwezi ukakitenganisha kamwe ukitenganisha jibu litakuja tofauti kama imejumuishwa na hesabu nyingine. Na hakuna haja ya kuweka mabano mengine kama hivi (x(ax+y)) ikisimama hivyo ilivyo inajieleza kabisa
 
Kama nje ya bracket hakuna tendo basi hakuna haja ya kweka mabano mengine

Ukishawekewa hivi 2(2+1) jua hicho ni kitu kimoja, wakati wa kufungua mabano lazima hiyo mbili ya nje iingie ndani ya hayo mabano ndio ufungue mabano, huwezi ukafungua mabano bila kuihusisha hiyo mbili ya nje.
Nje ya bracket hakuna tendo?
 
Hii 2(2+1) ni sawa na kusema (2+1)+(2+1) imerahisishwa tu
Lakini 2×(2+1) inabaki kama ilivyo, Japo vyote vitaleta jibu sawa
Tuishie hapo tu naona una matatizo yako special, sasa kama expansion form ya kidato cha pili sijui cha kwanza zimekupiga knock out chochote nitakachokueleza kimekuzidi umri.

2(2+1) expansio form yake ni (2×2) + (2×1) wala sio utumbo ulio andika hapo juu. Vile vile hii 2×(2+1) ipo kwenye factor form kama 2(2+1) na inaweza kua expanded kama nyenzie (2×2) + (2×1). Kitendo cha kuniambia haibadiliki napata mashaka na uwezo wako wa hesabu 😂😂😂.

Acheni ujuaji kama kitu hamjui kaeni chini mskilize mjifunze. Kama mtu hata kujua expression uliyopewa ni factorized au expanded form unajinasibu vipi na hesabu mmmh?

Kingine hata swali langu hukujibu, badili hizo numerical expression to words expression, umeuchuna kwa aibu kwasababu hujui chochote hapo.
 
Simu ipo sahihi zaidi (Jibu la calculator ni ya miaka ya 1917 so ni Wrong)

(3) inamaanisha thamani 2×3, ambayo ni 6. Kisha mlinganyo ni 6÷2×3. Kulingana na BODMAS ya kisasa, kuzidisha hakuji kabla ya mgawanyiko; Sheria inasema tuanzia kushoto kwenda kulia
6÷2 ni 3, na 3×3 ni 9. Kwa hivyo, jibu ni 9.
(According to modern interpretation of BODMAS)
Bodmas stands for B-Brackets, O-Orders (powers/indices or roots), D-Division, M-Multiplication, A-Addition, S-Subtraction
 
Tuishie hapo tu naona una matatizo yako special, sasa kama expansion form ya kidato cha pili sijui cha kwanza zimekupiga knock out chochpte nitakachokueleza kimekuzidi umri.

2(2÷1) expansio form yake ni (2×2) + (2×1) wala sio utumbo ulio andika hapo juu. Vile vile hii 2×(2+1) ipo kwenye factor form kama 2(2+1) na inaweza kua expanded kama nyenzie (2×2) + (2×1). Kitendo cha kuniambia haibadiliki napata mashaka na uwezo wako wa hesabu 😂😂😂.

Acheni ujuaji kama kitu hamjui kaeni chini mskilize mjifunze. Kama mtu hata kujua expression uliyopewa ni factorized au expanded form unajinasibu vipi na hesabu mmmh?

Kingine hata swali langu hukujibu, badili hizo numerical expression to words expression, umeuchuna kwa aibu kwasababu hujui chochote hapo.
ndo maana hesabu zikaandikwa kwa namba na sio maneno, wewe kaa na jibu lako na mimi nikae na langu, Na ndo maana scientific calculator original (ambayo siyo fake) itakuletea jibu 1 kwakua ile imeundwa kwaajili ya calculation kwaiyo inakwepa makosa yote ya kimahesabu. ila calculator ya simu ile ni ziada tu inaweza ikaleta majibu tofauti kwakua sio kazi ya simu kufanya calculation.

Kwa ninavyokuona hatuwezi kufikia huu maelewano kwenye huu mjadala ni sawa na 6 mkiwa wawili pande tofauti kuna atakayeona ni tisa na mweingine ni sita. kwaiyo huenda wote tupo sahihi kutokana na upande tuliokaa.
 
Simu ipo sahihi zaidi (Jibu la calculator ni ya miaka ya 1917 so ni Wrong)

(3) inamaanisha thamani 2×3, ambayo ni 6. Kisha mlinganyo ni 6÷2×3. Kulingana na BODMAS ya kisasa, kuzidisha hakuji kabla ya mgawanyiko; Sheria inasema tuanzia kushoto kwenda kulia
6÷2 ni 3, na 3×3 ni 9. Kwa hivyo, jibu ni 9.
(According to modern interpretation of BODMAS)
Bodmas stands for B-Brackets, O-Orders (powers/indices or roots), D-Division, M-Multiplication, A-Addition, S-Subtraction
Ofcourse jibu la Calculator linafata Rule ya a÷2(b) kua ni sawa na a/(2b). Wala haikukiuka BODMAS rule. Isipokuwa kwenye hicho kiji'expression

Ilipofika kwenye 6÷2 (3) ikaifanya kama 6/(2 ×3), then 6/6 mwisho 1. Kitu ambacho hakipo kwenye modern mathematics. Ambapo 6 ÷ 2 (3) ni sawa na 6 ÷ 2 × 3 inaleta 9.
 
ndo maana hesabu zikaandikwa kwa namba na sio maneno, wewe kaa na jibu lako na mimi nikae na langu, Na ndo maana scientific calculator original (ambayo siyo fake) itakuletea jibu 1 kwakua ile imeundwa kwaajili ya calculation kwaiyo inakwepa makosa yote ya kimahesabu. ila calculator ya simu ile ni ziada tu inaweza ikaleta majibu tofauti kwakua sio kazi ya simu kufanya calculation.

Kwa ninavyokuona hatuwezi kufikia huu maelewano kwenye huu mjadala ni sawa na 6 mkiwa wawili pande tofauti kuna atakayeona ni tisa na mweingine ni sita. kwaiyo huenda wote tupo sahihi kutokana na upande tuliokaa.
Uko mweupe sana kwenye mathematics, kila kauli unayo itoa inaonenya ni jinsi gani kwenye huu ukurasa haujui au umekariri kupindukia.

ndo maana hesabu zikaandikwa kwa namba na sio maneno,
Yes nikisea unakariri sijakosea. Number ni symbol of communication kama zilivyo herufi. Wakati wengine wana 1 hadi 9 warumi nao wanazo za muundo wao na waarabu vivyo hivyo.

Sentensi kama "Tulikuwa watu saba kati yetu wanawake wawili wanaume watano" katika number inawezwa kuandikwa hivi 7 = 2 + 5. Ya kwanza ndio tunaita words expression na ya pili tunaita numerical expression zote zina convey the same meaning.

1 hadi 9 na A hadi Z ni alama za mawasiliano na zinapatikana popote kwenye aina yoyote ya taaluma. Matendo kama kupunguza (kutoa), kuongeza (kujumlisha) ndio yanayoleta neno hesabu.

In words expression "Juma alimpa Jesca kalamu nane kati ya 20 alizokuwa nazo, aliongeza kalamu zingine kumi na tano kabla hajazigawa kwa kila mmoja kwenye familia ya watu tisa kwa usawa hivo hivo kila mmoja alipata kalamu 3"... in numerical expression inakuwa
[{(20-8)+15}÷9] = 3.

One mistake tu kwenye numerical expression either kwa wrong placement ya mabano inabadili maana totally. Mfano kwa hapo juu numerical expression kama hii
[(20-8)+15÷9] haileti 3 ambayo ni jibu la maana iliyokusudiwa mwanzo ingawa number zilizotumika ni zile zile na operational symbol ni zile zile zinazohitajika kasoro brackets husika hazipo...

Lengo la kubadili Words to numerical au numerical back to words expression ni kutest validity ya maana iliyokusudiwa kama haijabadilika ili kupata usahihi wa kinachotafutwa.

Kila numerical equation ina majibu ila si kila jibu lina reflect maana iliyokusudiwa. Na hiyo ndio hesabu sasa. Sio mikunjo ya 123 hadi 10.

So tusipeane mzigo wa kuanza kufundishana hesabu ni nini. Ukitaka kujua zaidi mwanao kwanini mwalim wake wa hesabu anamwambia ahesabu number kisha aziandike kwa maneno.

Na ndo maana scientific calculator original (ambayo siyo fake) itakuletea jibu 1 kwakua ile imeundwa kwaajili ya calculation kwaiyo inakwepa makosa yote ya kimahesabu
Again tena hii inaonesha hata neno Calculator hulijui maana ake.

Calculator/Kikotoo ni kifaa kinacho-perfom calculation/ukokotoaji under specific instructions. Vikokokotozi kama hicho unachodai kua ni Og sio fake kile ni programmable device ambacho kina perfom calculation under specific instructions.

All modern calculators hazitumii standard hiyo iliyo kuepo enzi hizo za 1917 that a÷b(c) ni sawa a/(b×c).

Kitendo cha kusema imeundwa maana ake unatakiwa uelewe iko programmed. Kua programmed ni kupewa set of instructions za ku'execute kwa kila command inayotolewa.

So when rules changed basi na outcome inabadilishwa kwa mfano lel say kule value of pie ilikuwa 20/7 (hii value ya mfano tu) but now ni 22/7. For the same calculation itakupa majibu tofauti kwasababu zinapokea command na ku'execute taarifa kwa instructions tofauti.

calculator ya simu ile ni ziada tu inaweza ikaleta majibu tofauti kwakua sio kazi ya simu kufanya calculation.
Sentensi kama hizi ndio zinaonesha hata kile unacho kizungumza hukijui. Tuacheni ubishi badala yake tukae chini tujifunze tuelewe.

Leo ukichukua vipimo vya uingereza ukaenda kuvi-apply US vinakuingiza chaka kwasababu wanatumia standard tofauti. Hapo juu nilitoa mfano wa Gallon kwa Litre.

Ukichukua Calculator ambayo iko programmed kwa standard za UK ambapo 1 Gallon kwa 4.546Litre ukaitumie US ambapo standard zao ni 1 Gallon kwa 3.872Litre itakuaje?

Utaiita fake au?

TUJIFUNZE KUELEWA.

Huku kukariri kwetu bila uelewa ndio unaofanya tukitoka nje ya mipaka yetu tunakuwa USELESS.
 
Wewe ndiye unayehitaji maombi.

Unayo machungwa sita na unataka uyawagawie makundi mawili ya idadi ya watu waliomo waliomo ndani ya mabano je kila mtu atapata machungwa mangapi??

1---- Machungwa 6,
2----Idadi ya makundi 2.
3---Idadi ya Watu katika kila kundi ( 2+1)=3.
4--- Jumla ya watu 6.
5---kila mtu atapata machungwa mangapi??, idadi ya machungwa÷ idadi ya watu = kila mmoja atapata chungwa moja.

Mathematical representation ya jambo hilo ni hii hapa:-

6÷[2(2+1)]=1. na sio 6÷2(2+1).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Safi mkuu,

Hawa watakuwa wale vilaza wa Magu wa pale UDOM nini?
 
Back
Top Bottom