Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Usiku siwezi kukimbiza sana.

Naingiwa na woga tu. Halafu sioni mbali sana.

Mchana unaweza kuona hata 1Km kama ni tambarare kwahiyo unapimia kabisa.

Ila usiku maximum 500M. Ambayo ni ndogo sana kwa mimi kufanya sudden decision ukiwa above 150kph.
Sababu ulizotaka ndio zinanifanya niepuke safari za usiku.
 
Nilishawahi drive Carina Ti 1500cc to 140km/hr gari ikawa inaanza kukosa stability,Swali nililojiuliza ni Je,itakuwaje kwa mtu anayeendesha Carina Ti 2200cc ambayo i think ni Turbo charged akaenda 180km/hr sijawah pata majibu.
Ni kwasababu ushaendesha gari ingine stable zaidi. Kama mtu gari yake ni hio hio Carina anaamini hakuna gari stable kama yake.
 
Sababu ulizotaka ndio zinanifanya niepuke safari za usiku.
Kuna siku nasafiri usiku, nikaona chombo mbele yangu kina taa moja, nikadhani ni pikipiki.

Hamadi mita kama 50 naona ni gari ina mzigo.

Niliyumba siku ile sitasahau, sio kwa kumkwepa vile.

Siku nyingine maeneo ya mwanga, chombo hakina taa nyuma.

Nagundua ni trekta limebeba mazao nimeshafika mita kama 50 hivi. Nikamkwepa nikavaa tuta.

Nimetokea kuchukia sana kusafiri usiku. Hasa hizi barabara zetu huchelewi kukuta kundi la ng'ombe au mbuzi barabarani na upo zako 170kph.

Ndo utajua hujui.
 
Sitakaa nimsahau yule trafiki.

Na kwa wenge nikasahau hadi leseni yangu kwake.
Jamaa yangu we kiboko-Traffic anatumia taratibu gani kukuandikia?Anayestahili kupima ni nan? atapimaje ajali bila kufika tukio husika? jam inasababishwaje na aliyegongwa mpaka apigwe fain? kweli hamna namna 🤣🤣-Traffic alivyofika kituoni lazima alihadithia wengine encounter yako😁😁😁
 
Madalali ni makuzi sana basi tu.
 
Yule mhuni wa Arusha Speedometer yake ya Aristo ni 180km/h ila ikipigwa speedgun top speed inasoma 300km/h.

Mambo ya modes hayo.

Kufika top speed ya 300km/h sio mchezo kabisa kabisa,hata hizi Germany machines nyingi zina speedometer ya 260km/-300km/h lkn unakuta top speed yake ya ukweli ni 240-250km/h hapo ndo mwisho.
 
Hii ya trekta isiyo na taa wala reflector nyuma nilikutana nayo mida ya saa moja usiku karibu na Nangurukuru, halafu upande wa pili naona taa za chuma inakuja. Siku ile nilikanyaga break nikaja kusimama kama mita 5 hivi kutoka kwenye trekta. Bahati nzuri nilikiwa just 100-120kph. Sipendi kabisa safari za usiku. Nasafiri usiku ikibidi tu na hapo speed mwisho 120.
 
Hapo ndipo ule msemo wa 'If it ain't broke don't fix it' unapo play part yake.
 
Yule ni mwamba,mbali na hiyo Aristo yenye 2gzte ana ile Chaser tourer nayo ni hatari,cha kushangaza kwa muonekano ni gari ya kawaida ila sokoni bei inagonga usd 20,000 bila cif
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…