Jamaa yangu we kiboko-Traffic anatumia taratibu gani kukuandikia?Anayestahili kupima ni nan? atapimaje ajali bila kufika tukio husika? jam inasababishwaje na aliyegongwa mpaka apigwe fain? kweli hamna namna [emoji1787][emoji1787]-Traffic alivyofika kituoni lazima alihadithia wengine encounter yako[emoji16][emoji16][emoji16]
Ndo mara yangu ya kwanza kupata ajali.
Lilikuwa wenge.
Baada ya ajali nikasubiri aje kupika. Nikaona anachorachora chini na kuhamia kwenye karatasi.
Baada ya hapo akaniambia niondoe gari tukamalizane na alienigonga. Nikamwambia hakuna kumalizana wakati ana bima. Mzigo ukalipwe na bima.
Akasema kitu kidogo mpaka msumbuane mahakamani? Nikamwambia kazi ya bima ni nini? Nikamwambia huyo jamaa hana uwezo wa kulipa matengenezo ya ile gari.
Yule jamaa akasema tumalizane. Nikamwambia kama kumalizana tunaenda garage, estimation zote utalipa kabisa ndo unaondoka.
Polisi akasema tuondoe magari yetu barabarani. Tukapeleka pale pembeni ya kibanda chao.
Kufika pale polisi ndo akanigeuka. Nimesababisha foleni.
Mabishano ndo yakahama toka kugongwa mpaka kusababisha foleni. Alienigonga akataka anipe 50K yaishe.
Kufupisha, tulibishana masaa mawili mazima. Akachukua leseni yangu akaingia kwenye kibanda chake akarudi na risiti ya fine. Sikuwaza tena kama nilimpa leseni. Sikumtafuta tena. Nikarenew baada ya kama miaka miwili hivi. Na ile fine sikuilipa mapaka dec 2020 walivyonikagua na vikamera vyao barabarani.
Yule jamaa ilibidi tupelekane garage. Akapewa estimation za matengenezo akalipa nusu na kuacha simu yake. Akaja kumalizia baada ya wiki hivi. Ambapo bima ingemlipia kirahisi sana.
Toka siku hiyo. Polisi nawaweka kundi moja na wanyama. Siwezi nikapata shida nikawapelekea polisi nitatatua mwenyewe.