Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Na ile migongo kama tank haina shield unalitoboa chap tu.
 
Na ile migongo kama tank haina shield unalitoboa chap tu.
Laiti barabaraba zote nchi hii zingekua na hali kama ya mkeka wa Tunduru - Songea, ama Dom - Kondoa - Babati - Arsh, Ama Igawa - Mafinga, safari zingekua starehe kwa wote dereva na abiria. Ila udereva wetu ni mahangaiko kweli kweli na iliqa ni usiku ndio mbaya zaidi, pot holes zisizotarajiwa, sharp humps daah

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
ongeza tunduru-masasi, njombe-makambako
 
Niliwasikia watu pale feri leo wanaiongelea hiyo kwamba kuna njia fupi ila rough road. So lami bado.
Ile barabara ni fupi, ila gari lazima uichoshe ni barabara mbaya sana. Japo nakumbuka JPM alitoa maelekezo kwa Eng Mfugale ijengwe kipindi cha kampeni. Nahisi inaweza ikawa kwenye michakato
 
Ongeza Shinyanga - Lamadi via Maswa / Bariadi
 
Ongeza Shinyanga - Lamadi via Maswa / Bariadi
Sasa tunahitaji sana consistency kwenye ubora wa barabara zetu hizi kuanzia miradi mipya mpaka maintenance ya zilizopo zinazosimamiwa na Tanroads ndani ya mkoa mmoja hadi mkoa hadi mkoa. Mfano rahisi before kipindi cha kampeni barabara ya Dom - Mtera ilikua na mahandaki ya kufa mtu, same Tanroad mkoa ndio inasimamia Dom - Moro, Dom - Bahi, na Dom - Kondoa. Sasa hii ya Kondoa ni mpya so case yake ni tofauti kidogo, but hii ya Bahi na Dom -Gairo since zapitwa sana na wakubwa No. 1 included as barabara ndio namna yake pendwa zaidi ya kusafiri zimekua zikiangaliwa sana, tofauti na ile ya Dom - Mtera ni kama ilitelekezwa despite umuhimu wake (kiunganshi cha so called Great North Corridor - Cape Town - Cairo)
 
Nimetokea kuichukia morogoro road.

Bora nikazungukie bagamoyo nikatishe msoga.

Ila kipande cha chalinze-mbezi mwisho sikipendi kufa.
 
Sipende overtaking ya hapa na hapa.

Infact siziwezi kabisa.

Niki-overtake lazima nikuanzie mbali, hata kama gari ni 10 nazipiga zote.

Ila hii ya kuchomoa hapa na hapa siiwezi.
 
Nimetokea kuichukia morogoro road.

Bora nikazungukie bagamoyo nikatishe msoga.

Ila kipande cha chalinze-mbezi mwisho sikipendi kufa.
This mostly favors mtokeao maeneo close to Bagamoyo Road (Goba, Kawe, Mbezi Beach, Ununio, Tegeta, Mbweni n.k) Atokeae Tabata, Kitunda, Kinyerezi, Chang'ombe n.k akishapenya na Kifuru Malamba Mawili akatokea Mbezi heri akomae tu na Morogoro Rd aitafute Chalinze kwa mbinde kuliko mzunguko wa kuitafuta Bagamoyo Rd na foleni zake hadi afike Msata hoiiii

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Sipende overtaking ya hapa na hapa.

Infact siziwezi kabisa.

Niki-overtake lazima nikuanzie mbali, hata kama gari ni 10 nazipiga zote.

Ila hii ya kuchomoa hapa na hapa siiwezi.
Kuna muda unalazimika kupangua mmoja mmoja huku unaendelea kupunguza umbali maana hapo pa kuwapangua 5 na zaidi kwa pamoja itabidi usubiri umbali mrefu sana at times

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Hivi mnapataga muda wa kusalimianaga na kuulizana kuhusu magari yenu?
 
Hivi mnapataga muda wa kusalimianaga na kuulizana kuhusu magari yenu?
Hii ni kawaida, kama ni route ya Dar - Moro - Iringa - Makambako, refueling stations na kuchimba dawa iwapo upo na familia zaweza kuwa points mnazowezakutana na kusemeshana. Kwa ruti hiyo Morogoro Total pale Msamvu, Total Mikumi ama Iringa pale Ipogolo weng huweka kituo briefly kabla ya kulisongesha. So kama mliburuzana sana huko nyuma si haba kusema 'hello' ha ha ha na salute ya heshima if need be kama umenyooshwa 😀 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…