Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Pole sana Mkuu kwa kukoswakoswa na ajali bora hata ungejisogeza bondeni uwaachie barabara kabisa kwani alioa wewe sio size yake kwa vile gari yako ina umbo dogo kuliko Lori
na ungekuwa na bastola na ukamfukuza mwenye Lori ungewekwa Kituoni Kabuku mambo yangeharibika kabisa.
Kukaa barabarani ni elimu tosha, mm kuna jamaa alikula wrong site kwenye mzunguko wa keep left akanivaa na kuharibu gari yangu, Traffic wakaja wakamshauri akanitengenezee nikakubali kufika gereji bado alishindwa nikamalizia mwenyewe bora Uhai Mkuu
Mkuu unashuka unazitwanga tyre zake zote alale porini.. sio yeye alafu unaondoka zako
 
IMG_20210228_124802_1.jpg
 
Jana usiku kabla ya Kabuku kuna mwenye lori ilikuwa atuue. Ingekuwa nimewahi sekunde tano tu leo nisingekuwa hapa naandika haya.
Ilikuwa kwenye kona na kwasababu giza lilishaingia nilikuwa mwendo fulani mdogo around 80kph nikaipita bodaboda inatembea pembeni.
Mbele kidogo naibuka kwenye kona naona Mita kadhaa mbele malori mawili yanaligi yananijia moja imejaa kwangu ilikuwa head-on collision! Nikawahi kufunga breki kali Lori linakuja tu nikaitoa gari pembeni ya barabara natizama bonde. Mwenye lori alikuja hadi Mita kama mbili tu akamlazimisha mwenzie akamchomekea kunikwepa mimi.
Wakati nahangaika hivi bodaboda nyuma yangu hajui nini kinaendelea akaniovateki akakutana na lori ikabidi yeye na abiria wake waingie kwenye bonde! Lori likaendelea na safari. Bodaboda waliinuka ila waliumia maana niliona wanachechemea huku wakijishika viuno! Mungu mkubwa.
Pole sana pal........hakika kutokuwa muoga kulikusaidia
 
Leo imetokea jioni njia ya mbagala-kongowe

Roli lililobeba lami lilikua linashusha mlima likafeli breki..chini ya mlima kulikua na gari tatu zinapanda ya kwanza tank la mafuta,ya pili canter ya mafuta pia na canter ya kawaida ....Mwenye roli la lami baada ya kuona breki zimefeli akawasha taa fulu ,,yule mwenye tank akawa ameshamsoma akampisha lakini akawa amechelewa akagongwa uso kwa uso ila upande wa abiria na pia lile lori zikavamia na gari za nyuma zile canter likaanguka hapo ...so ajali ya gari nne kwa wakati mmoja.

Nb:tetesi zinasema wamekufa wawili,,dereva na utingo wa lori la lami walirukaView attachment 1713473View attachment 1713479

Nimesikia ni Simiyu
Hatari sana, Mungu atuongoze kwa kweli.
Tatizo watu wengi hawajui kuwa kupata ajali sio lazima uwe umefanya kosa
 
Mkuu Crown iliopiga mzinga Dodoma recently watu wanne walikufa hapo hapo. Alipona mmoja abiria alikaa mbele.
My point ukipiga kishindo heavy na lori au bus kupona ni majaliwa uwe mbele au nyuma.
Ilikuwa nyeupe sio? Kama 2 weeks ago? Nilipita alfajiri nilikuwa naenda Moro, nikaiona imewekwa pembeni imeisha vibaya mno nikajisemea wamekufa watu bila shaka maana imebonyea mpaka nyuma.

Aliipiga wapi ile gari?
 
Jana usiku kabla ya Kabuku kuna mwenye lori ilikuwa atuue. Ingekuwa nimewahi sekunde tano tu leo nisingekuwa hapa naandika haya.
Ilikuwa kwenye kona na kwasababu giza lilishaingia nilikuwa mwendo fulani mdogo around 80kph nikaipita bodaboda inatembea pembeni.
Mbele kidogo naibuka kwenye kona naona Mita kadhaa mbele malori mawili yanaligi yananijia moja imejaa kwangu ilikuwa head-on collision! Nikawahi kufunga breki kali Lori linakuja tu nikaitoa gari pembeni ya barabara natizama bonde. Mwenye lori alikuja hadi Mita kama mbili tu akamlazimisha mwenzie akamchomekea kunikwepa mimi.
Wakati nahangaika hivi bodaboda nyuma yangu hajui nini kinaendelea akaniovateki akakutana na lori ikabidi yeye na abiria wake waingie kwenye bonde! Lori likaendelea na safari. Bodaboda waliinuka ila waliumia maana niliona wanachechemea huku wakijishika viuno! Mungu mkubwa.
Ila Bongo kwa kweli Mungu huwa anatuongoza tu nyakati nyingine, na hizi alama zetu za majani barabarani tena wakati mwingine wayakuta ndani ya umbali mfupi kweli kufikia kilipo kicheche/tatizo mmmh. Moja nishaikutaga Bwawani pale usiku kama saa 5 na ushee hivi nimepandisha tu kuelekea Moro jamaa ndio wametoka kupasuana luckily kuna waliokua barabarani kutahadharisha madereva wengine kwa tochi ili wapunguze mwendo ilisaidia sana ile maana pale wengi huwa wanapanda nayo nzima nzima aisee. By the way nimejifunza nafikiri pia ni muhimu sana kuwa na tochi ya tahadhari kwenye gari aisee sio nyakati zote tochi ya kwenye simu itafaa.
Usiku + Vicheche ni combination moja hatari sana.

Last trip nilikuwa nimeiva usiku kwenye saa 4 naitafuta Sekenke, hakuna gari mbele yangu, ukatokea msururu wa magari kutoka upande wa pili tupishane nao, wa mbele akawa ananiflashia high beam constantly japo nilishazima high beams, nikaanza kupunguza mwendo na kuwa attentive.

Kumbe kuna kicheche mbele yangu, yeye alikotoka amekiona anajaribu kunishtua, sasa kinyume chake yale mataa yake yakawa yananitoa kwenye focus kuangalia mbele yangu naishia kuhangaika na flashes zake, kuja kushtuka majani haya hapa! Bahati nzuri nakaaga katikati ya barabara so nikayakwepa na niliyavaa kiaina nikawa nasikia harufu yake ndani ya gari.

Kunisaidia angeflash mara moja na kuzima taa nione vizuri. Kumflash mtu mara kumi kumi kwamba kuna kicheche mbele ndio kabisa unamzuia kukiona.

Kupishana usiku at high speed ni sanaa ya aina yake
 
Back
Top Bottom