RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
- Thread starter
- #3,521
Kuna vicheche vinaachwa kwenye mazingira hatarishi sana, giza likiingia barabara zetu hizi ni hatari sana. Kuna Mzee wa usiku Kwa usiku simuoni humuUsiku + Vicheche ni combination moja hatari sana.
Last trip nilikuwa nimeiva usiku kwenye saa 4 naitafuta Sekenke, hakuna gari mbele yangu, ukatokea msururu wa magari kutoka upande wa pili tupishane nao, wa mbele akawa ananiflashia high beam constantly japo nilishazima high beams, nikaanza kupunguza mwendo na kuwa attentive.
Kumbe kuna kicheche mbele yangu, yeye alikotoka amekiona anajaribu kunishtua, sasa kinyume chake yale mataa yake yakawa yananitoa kwenye focus kuangalia mbele yangu naishia kuhangaika na flashes zake, kuja kushtuka majani haya hapa! Bahati nzuri nakaaga katikati ya barabara so nikayakwepa na niliyavaa kiaina nikawa nasikia harufu yake ndani ya gari.
Kunisaidia angeflash mara moja na kuzima taa nione vizuri. Kumflash mtu mara kumi kumi kwamba kuna kicheche mbele ndio kabisa unamzuia kukiona.
Kupishana usiku at high speed ni sanaa ya aina yake
East Wind