Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mkuu unashuka unazitwanga tyre zake zote alale porini.. sio yeye alafu unaondoka zako
 
Pole sana pal........hakika kutokuwa muoga kulikusaidia
 

Nimesikia ni Simiyu
Hatari sana, Mungu atuongoze kwa kweli.
Tatizo watu wengi hawajui kuwa kupata ajali sio lazima uwe umefanya kosa
 
Mkuu Crown iliopiga mzinga Dodoma recently watu wanne walikufa hapo hapo. Alipona mmoja abiria alikaa mbele.
My point ukipiga kishindo heavy na lori au bus kupona ni majaliwa uwe mbele au nyuma.
Ilikuwa nyeupe sio? Kama 2 weeks ago? Nilipita alfajiri nilikuwa naenda Moro, nikaiona imewekwa pembeni imeisha vibaya mno nikajisemea wamekufa watu bila shaka maana imebonyea mpaka nyuma.

Aliipiga wapi ile gari?
 
Usiku + Vicheche ni combination moja hatari sana.

Last trip nilikuwa nimeiva usiku kwenye saa 4 naitafuta Sekenke, hakuna gari mbele yangu, ukatokea msururu wa magari kutoka upande wa pili tupishane nao, wa mbele akawa ananiflashia high beam constantly japo nilishazima high beams, nikaanza kupunguza mwendo na kuwa attentive.

Kumbe kuna kicheche mbele yangu, yeye alikotoka amekiona anajaribu kunishtua, sasa kinyume chake yale mataa yake yakawa yananitoa kwenye focus kuangalia mbele yangu naishia kuhangaika na flashes zake, kuja kushtuka majani haya hapa! Bahati nzuri nakaaga katikati ya barabara so nikayakwepa na niliyavaa kiaina nikawa nasikia harufu yake ndani ya gari.

Kunisaidia angeflash mara moja na kuzima taa nione vizuri. Kumflash mtu mara kumi kumi kwamba kuna kicheche mbele ndio kabisa unamzuia kukiona.

Kupishana usiku at high speed ni sanaa ya aina yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…