Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Bado unaamini kufungua vioo unaokoa mafuta?
Nilishajaribu huko nyuma na nilihakiki ni kweli kwa road trip nayotembea maana foleni ni nyingi.
Nikitembea na AC kwa wiki (150 KM) inaongezeka gharama ya mafuta kati ya 4000-8000 ya kipindi hicho.
Lakini nikaangalia faida za kufungua madirisha na kusave mafuta na faida za kufunga muda wote kama vile gari kuwa safi muda wote, kuitendea haki tinted, kuto panic gari la pembeni likiingia kwenye dimbwi kwa speed, bajeti ya mafuta kuwa stable hata kipindi cha mvua (hapa utake usitake utawasha AC tu)
 
Watu wanasema AC inamaliza mafuta, ingawa sionagintofauti sana, nahisi na akili zimeisha kalili
AC inamaliza mafuta kama gari imesimama. Gari ikisimama hata mlio utasikia unaongezeka ili kusukuma compressor (rpm inapanda juu ya normal idle). Ila gari ikitembea inatumia mzunguko wa kawaida wa engine na in fact kufungua vioo wakati gari inaenda unatumia mafuta zaidi kwasababu ya drag inayosababishwa na upepo.
 
Binafsi huwa naamini source ya power kwenye gari huwa generated na engine kupitia mafuta.A/C inapowaka inafanya alternator kufanya kazi,na alternator source yake ya power ni engine,na engine hupata hiyo power kwa kuchoma extra fuel.
Based on researches
-Kuna certain speed wakati unaendesha,gari linakuwa more fuel efficient with A/C on kuliko gari lililofunguliwa vioo at that speed.
*Binafsi nilicho notice kwenye gari, ni kwamba nikiwasha headlights especially full lights mngurumo wa engine hubadilika hasa gari ikiwa kwenye silencer,hii ni indication kwamba load kwenye engine imeongezeka kwa kiasi fulani,And this increased engine load inakuwa compesated na kuongezeka kwa uchomaji kidogo wa mafuta-ingawa naamini ni kwa kiwango kidogo mnoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…