Bahati yako mkuu, juzi natoka Moro kuna mbwa alitaka atuue maeneo ya Mlandizi. Nilikuwa kwenye Mazda hatchback flani ya 2009 ya jamaa anatembea japo kwa kuvizia vizia. Tuko mahali pamenyooka tumelikata Truck mbele kuna RunX imekaza jamaa akaikazia mguu nayo. Kama sekunde 15 tushaimaliza RunX tunarudi site mita 10 mbele kuna shoga ghafla kaitoa Scania ya mafuta sheli anaitaftia kona kaambaa barabara nzima kaacha kama nafasi ya mita moja toka ukingoni.
Kilichotokea mzee baba acha tu, jamaa ilibidi akaze roho. Akaitolea pembeni nako kulikuwa na ngema ikaparuza uvungu kisha akairudisha juu maana kulikuwa na tofali la zege linafata. Ndio pona yetu angekuwa muoga angeipiga Scania ubavuni.
Tukakubaliana aache fujo, kituo kinachofata tunakuta kuna jamaa kala buyu. Noah mayai kaipiga fuso vizuri tu mpaka katatua Airbag, Fuso imedondoka miguu juu kichwa chini kwenye korongo.