Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Honestly nilikuwa speed fulani ndogo kwasababu giza lilishaingia. Ila ingekuwa yale mambo yetu ya 150kph saa hizi yangekuwa mengine.
Bahati yako mkuu, juzi natoka Moro kuna mbwa alitaka atuue maeneo ya Mlandizi. Nilikuwa kwenye Mazda hatchback flani ya 2009 ya jamaa anatembea japo kwa kuvizia vizia. Tuko mahali pamenyooka tumelikata Truck mbele kuna RunX imekaza jamaa akaikazia mguu nayo. Kama sekunde 15 tushaimaliza RunX tunarudi site mita 10 mbele kuna shoga ghafla kaitoa Scania ya mafuta sheli anaitaftia kona kaambaa barabara nzima kaacha kama nafasi ya mita moja toka ukingoni.

Kilichotokea mzee baba acha tu, jamaa ilibidi akaze roho. Akaitolea pembeni nako kulikuwa na ngema ikaparuza uvungu kisha akairudisha juu maana kulikuwa na tofali la zege linafata. Ndio pona yetu angekuwa muoga angeipiga Scania ubavuni.

Tukakubaliana aache fujo, kituo kinachofata tunakuta kuna jamaa kala buyu. Noah mayai kaipiga fuso vizuri tu mpaka katatua Airbag, Fuso imedondoka miguu juu kichwa chini kwenye korongo.
 
Barabarani kuna ujinga mwingi sana. Halafu aliesababisha yote hayo kaendelea na safari wala hajali nini kimewatokea.
 
Kwani unafikiri wanaonyooshwa na ni hizo gari wanaangukia kundi gani? Vijana au wamiliki wa Kwanza. Wapo watu wazima wengi wana hizo gari ila hutasikia wamepata ajali kama tunazosikia za hao vijana.
Hizo gari zinatiaga wazimu sana highway 😁 mtu anajisahau anataka akate semi 4 kwenye blindspot akihisi atamaliza. Gari inataka nidhamu hasa uendeshaji wa Usiku. Zinachanganya haraka mno yani kwa engine 4GR Toyota alitengeneza.. Halafu kuna ile ya 3.0L 3GR nayo ni balaa..ndio mrithi wa 2JZ
 
Wamiliki wengi gari ya kwanza hawana utulivu, bado vijana. Ujana na nguvu ya Mark X au Crown ni combination ya hatari.
Btw ni hela yako tu yoyote ile unaweza kununua. Kwa wenzetu gharama za insurance zinategemea sana umri wako na aina ya gari.
Mtu kaotea hela anajikwapulia Mark X lake la 8M liko vizuri basi. Ni vurugu mechi tu siku 2-3 anajitafti safari tu. Very recklessly anaovertake kila gari ili mradi tu anaweza😁😁😁 bila kujali usalama
 
Hio Crown hakuna rangi itaacha ona...mishale ya dashboard yote itagusa sehemu ambayo haijawahi kugusa!
Vijana lazma waipimp kisha watasumbua sana. Kuna mwanangu chizi Brevis sahizi kahamia kwenye Crown rasmi.

Kila gari akishaitoa bandarin lazma apige ruti ya Moro-Arusha anakwambia anaitoa mafua😂 na antembeaga kweli kweli😂!
Yani akimka saa 9 Moro ikifika saa 2 asubuhi anakupigia yuko Moshi mjini mkapige supu mahali.

Sasa kaagiza Royal Salon 3.0L 3GR Machine 😂 GRS180!
Mwanzo aliwahi kununua lile GRS202 model ya 2009 mwanzoni akakamua nalo masaa 5 nikamnyooshea mikono juu aisee saa 1 yuko getini kwangu.
 
Naombeni kujua kama nina IST nipo mimi na mpenzi wangu (2 tu), natoka DAR naenda kumfata KILOMBELO, then tutatoka KILOMBELO to MOSHI, ni mara ya kwanza kufanya ivyo je mfukoni natakiwa niwe na sh ngapi plus mafuta???
 
Wazee wa safari, wapi hapa?
 
Attachments

  • 2EE74629-FD36-4210-8499-54263953C0D7.jpeg
    2EE74629-FD36-4210-8499-54263953C0D7.jpeg
    32.9 KB · Views: 4
Naombeni kujua kama nina IST nipo mimi na mpenzi wangu (2 tu), natoka DAR naenda kumfata KILOMBELO, then tutatoka KILOMBELO to MOSHI, ni mara ya kwanza kufanya ivyo je mfukoni natakiwa niwe na sh ngapi plus mafuta???
Km ngapi hapo? Tumia Google kupata umbali.
 
Naombeni kujua kama nina IST nipo mimi na mpenzi wangu (2 tu), natoka DAR naenda kumfata KILOMBELO, then tutatoka KILOMBELO to MOSHI, ni mara ya kwanza kufanya ivyo je mfukoni natakiwa niwe na sh ngapi plus mafuta???
Kutoka Kilombero, ukifika Moro unakunjia Dom, Kondoa, Babati, Arusha Moshi for adventure ama wapitia Chalinze Segera Moshi?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
mkuu sijajua, maana ndio mara yangu ya kwanza kwenda uko
Muongozo wa google ni kusearch to Dar - Kilombero distance, then Kilombero - Moshi distance upate makadirio ya umbali wa safari yako tarajiwa. Kutoka ktk huo umbali ndio waweza fanya makadirio ya mahitaji ya mafuta

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom