Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mombasa ni karibu sana. Muda wa lunch anakuwa kashafika.
Sure...

Ila sasa dada ni mpambanaji nahisi Zimb walipomshauri watu wengine kutakuwa miyeyusho tu kwake, maana wale washaharibikiwa...atachofaidi ni adventure tu!!

Kuna ndugu yangu alikuwa kaoa halafu kaenda ishi huko, last two years karudisha mpira kwa kipa, hali mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilitoka Dodoma saa 2 usiku saa 9 tukaingia Mwanza, moja kwa moja the cask. Na palikuwa pamewaka vibaya mno.
[emoji4]

Mkorintho unaona balaa jingine hili, hivyo usishangae sana hiyo ya 7~8 hrs Mby-Dar...

Dom - Mwz ni kama 690 au 700km hivi, upungufu wa kama 115km tu ukilinganisha na safari ya Dar - Mby...

Hapo mtu katembea masaa 7, ina maana saa la 8 ingekuwa safari inaendelea angeweza malizia hizo 115km pengine kwa dk 40 hivi
 
Asante Mzee JBourne59 kwa kuleta picha ya hili chimbo

Mwezi unaoanza wiki kesho, nataka nipeleke ronya za kariakoo huko

Pana fursa sana huko, kisha december nianze utalii wa ndani kwa kutembelea mikoa yote nchini
 
Hapa matuta, rasta na mashimo lazima yavaliwe na dereva atakua sio mara ya kwanza kupita barabara hiyo
 
Asante Mzee JBourne59 kwa kuleta picha ya hili chimbo

Mwezi unaoanza wiki kesho, nataka nipeleke ronya za kariakoo huko

Pana fursa sana huko, kisha december nianze utalii wa ndani kwa kutembelea mikoa yote nchini
Nilikula sana kuku wa kienyeji kwa ugali wa muhogo, sijui kwanini hawapaboreshi na kuweka parking kubwa maana ukifika hapo lazima spidi irudi almost sifuri ndio ukatize kama huna uroho wa nyama, otherwise nawe utaweka foleni pembeni.
 
hakika ubungo sio ubungo ile, kibaha sio kibaha ile tena.
Kama ulikaririki makontena na mti wa muarobaini lazima uangukie pua
Mimi huko huwa sitembei bila mwenyeji..ntapotea mchana kweupe .
Halafu mimi ni mbovu wa kukariri njia..hili ni tatizo hadi huku kijijini ninakoishi nilishawahi potea njia ya kurudi home.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshafanya sana route za huko

Mbeya - Songwe (Tunduma) - Sumbawanga hadi Mpanda

Kutoka Mpanda hadi Tabora
Kutoka Mpanda hadi Kigoma via Uvinza.

Gari inatakiwa iwe vizuri, vinginevyo unaweza kuchelewa kupata msaada ikitikea breakdown.
Oh!
Ukipiga tena trip za huku post picha hapa.
Watu wa huku tunafarijika kuona watu wanakuja trmbelea mikoa yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ira-Mby Ni 380km
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…