Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mombasa ni karibu sana. Muda wa lunch anakuwa kashafika.
Sure...

Ila sasa dada ni mpambanaji nahisi Zimb walipomshauri watu wengine kutakuwa miyeyusho tu kwake, maana wale washaharibikiwa...atachofaidi ni adventure tu!!

Kuna ndugu yangu alikuwa kaoa halafu kaenda ishi huko, last two years karudisha mpira kwa kipa, hali mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilitoka Dodoma saa 2 usiku saa 9 tukaingia Mwanza, moja kwa moja the cask. Na palikuwa pamewaka vibaya mno.
[emoji4]

Mkorintho unaona balaa jingine hili, hivyo usishangae sana hiyo ya 7~8 hrs Mby-Dar...

Dom - Mwz ni kama 690 au 700km hivi, upungufu wa kama 115km tu ukilinganisha na safari ya Dar - Mby...

Hapo mtu katembea masaa 7, ina maana saa la 8 ingekuwa safari inaendelea angeweza malizia hizo 115km pengine kwa dk 40 hivi
 
Panaitwa "Chalinze" kama sikosei, katikati ya msitu huko Mpanda - Uvinza rd. Kuku choma, Nyama choma bei nafuu sana hapo! Wakimbizi walowezi kibao maeneo hayo.

Nikaliona moja ya basi ya kampuni kongwe Rukwa - Katavi - Tabora - KigomaView attachment 1800195
Asante Mzee JBourne59 kwa kuleta picha ya hili chimbo

Mwezi unaoanza wiki kesho, nataka nipeleke ronya za kariakoo huko

Pana fursa sana huko, kisha december nianze utalii wa ndani kwa kutembelea mikoa yote nchini
 
Dar - Iringa 4.5hrs, distance 490km approx
Iringa - Mbeya 3 to 3.5hrs, distance 334km approx
Muda ni usiku, gari engine ni V6/V8 (gari nyingine hizi zenye engine za kawaida ni 9 to 9.5hrs)
Dar to Mbeya, vituo vya mafuta ni viwili (Mikumi na Makambako)
Min speed 120kph na mwendo huu ni hadi kule Iyovi, Max speed kisahani chote sehemu zinazoruhusu kama Ruaha Mbuyuni, Makambako hadi Iringa, Moro hadi Chalinze, sehemu kama Mikumi unajitoa ufahamu ile 50kph yao ya usiku unafanya kama huijui...

Sehemu speed kidogo inapungua Kitonga wakati wa kupanda approx 70 to 80kph...

Chimala hadi maeneo ya Nsonyanga Mbeya sababu ya barabara ina madimbwi na mashimo...

Mlandizi hadi pale mbele kidogo ya daraja la juu la treni, barabara ina mawimbi hatari...

Hii ilikuwa achieved wakati hapo Picha ya ndege hawajabomoa barabara, Kingolwira/Kingolwira Magereza hawajaanza chimba barabara, Iyovi hawajaanza kupanua barabara...
Hapa matuta, rasta na mashimo lazima yavaliwe na dereva atakua sio mara ya kwanza kupita barabara hiyo
 
Asante Mzee JBourne59 kwa kuleta picha ya hili chimbo

Mwezi unaoanza wiki kesho, nataka nipeleke ronya za kariakoo huko

Pana fursa sana huko, kisha december nianze utalii wa ndani kwa kutembelea mikoa yote nchini
Nilikula sana kuku wa kienyeji kwa ugali wa muhogo, sijui kwanini hawapaboreshi na kuweka parking kubwa maana ukifika hapo lazima spidi irudi almost sifuri ndio ukatize kama huna uroho wa nyama, otherwise nawe utaweka foleni pembeni.
IMG-20210528-WA0075.jpg
IMG-20210528-WA0076.jpg
 
hakika ubungo sio ubungo ile, kibaha sio kibaha ile tena.
Kama ulikaririki makontena na mti wa muarobaini lazima uangukie pua
Mimi huko huwa sitembei bila mwenyeji..ntapotea mchana kweupe .
Halafu mimi ni mbovu wa kukariri njia..hili ni tatizo hadi huku kijijini ninakoishi nilishawahi potea njia ya kurudi home.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshafanya sana route za huko

Mbeya - Songwe (Tunduma) - Sumbawanga hadi Mpanda

Kutoka Mpanda hadi Tabora
Kutoka Mpanda hadi Kigoma via Uvinza.

Gari inatakiwa iwe vizuri, vinginevyo unaweza kuchelewa kupata msaada ikitikea breakdown.
Oh!
Ukipiga tena trip za huku post picha hapa.
Watu wa huku tunafarijika kuona watu wanakuja trmbelea mikoa yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana Maxi nimeweka hizo 180Mins kwa anayemwaga moto mwanzo mwisho na kufukia matuta ya Tanangozi, Rungemba, Ifunda sijui Nyololo kote huko [emoji23][emoji23]. Kumbuka Ir - Mby ni parefu kidooogo (334Kms) than Moro - Ir (300Kms) only advantage ni Ir - Mby mkeka wake ni mtamu zaidi kuliko Moro - Iringa.
Ira-Mby Ni 380km
 
Back
Top Bottom