Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Na mwenyekiti wa Nissan nipo hapa..[emoji41][emoji41]..Naunga mkono hoja
 
Nimeshawahi kutoka tabora saa moja asubuhi, saa kumi nikawa kibaha, na hapo nilikaa kama saa nzima Dodoma kwa ajili ya kula.. lakini mpaka kupita ubungo ilikua saa tatu usiku yani ile foleni siwez kuja kuisahau.. ilikua december 2019 na mnyama crown athlete
 
Nje ya mada kidogo..

Hivi unakutana na mtu unampa lift, unamshusha sehemu anayotaka kushukia, kisha anakuomba hela....Tena mwingine anasisitiza.." Hujawahi kunipa hela".

Wazee wa road trip, hii kitaalamu imeekaje .?[emoji848][emoji848]
 
Angeenda kampala UG kwa kupitia Arusha, Namanga, Nairobi, Kisumu, Busia, Jinja, Kampala.

Ila kwa wenzetu basi ni 24/7, hakuna kulala.

Nilipanda basi Jinja saa 10 jioni, saa 1 asubuhi tuko Namanga
 
Pale mikumi hatari sana kukatiza kwa speed zaidi ya 120

Wanyama ni wanyama tu

Unaweza kuona peupeee mara pAAAp, tembo anavuka, ama nyumbu, ama Nyati (sipati picha)
 
Wakuu ahlan wasalan!!
Nje kidogo ya mada nilikuwa naomba kujua utaratibu wa kuingia nchi jirani kama kenya na chombo binafsi cha usafiri kipi/docx gani natakiwa kuwa nayo zaidi ya ppt. Mwenye uzoefu hasa wa border ya holili/tarakea shukran
 
Kuna siku nilitoka Dodoma saa 2 usiku saa 9 tukaingia Mwanza, moja kwa moja the cask. Na palikuwa pamewaka vibaya mno.
The cask huwa kina waka sana.. kipindi cha nyuma kila weekend ilikuwa lazima niwepo pale.. naanzia alhamisi,.ijumaa hadi jumamosi.. naondoka jumapili 😀😀😀😀.. ila sasa hivi majukumu mengi sana
 
The cask huwa kina waka sana.. kipindi cha nyuma kila weekend ilikuwa lazima niwepo pale.. naanzia alhamisi,.ijumaa hadi jumamosi.. naondoka jumapili 😀😀😀😀.. ila sasa hivi majukumu mengi sana
Nilivyokuwa Mwanza nilikuwa nakaa sana hapo na pale nyuma villa park I guess kuna samaki na band
 
Wakuu ahlan wasalan!!
Nje kidogo ya mada nilikuwa naomba kujua utaratibu wa kuingia nchi jirani kama kenya na chombo binafsi cha usafiri kipi/docx gani natakiwa kuwa nayo zaidi ya ppt. Mwenye uzoefu hasa wa border ya holili/tarakea shukran
Kadi og na insurance ya comesa I think. Kwa sasa covid 19 negative test certificate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…