Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ira-Mby Ni 380km
Kanyaga twende...
Screenshot_20200525-173737.jpg
 
Mkuu Siri moja ya Nissan Patrol ukiwa off road ni comfortability. Ukiendesha L/Cruiser Hardtop, Defender au Pajero huwa hazina utulivu kama wa Nissan.

Hongera zimfikie mmiliki kwa kutunza, Nissan ni gari ya mjapani ambayo haitaki janja janja kama Toyota.
Na mwenyekiti wa Nissan nipo hapa..[emoji41][emoji41]..Naunga mkono hoja
 
Nimeshawahi kutoka tabora saa moja asubuhi, saa kumi nikawa kibaha, na hapo nilikaa kama saa nzima Dodoma kwa ajili ya kula.. lakini mpaka kupita ubungo ilikua saa tatu usiku yani ile foleni siwez kuja kuisahau.. ilikua december 2019 na mnyama crown athlete
 
Nje ya mada kidogo..

Hivi unakutana na mtu unampa lift, unamshusha sehemu anayotaka kushukia, kisha anakuomba hela....Tena mwingine anasisitiza.." Hujawahi kunipa hela".

Wazee wa road trip, hii kitaalamu imeekaje .?[emoji848][emoji848]
 
Sure...

Ila sasa dada ni mpambanaji nahisi Zimb walipomshauri watu wengine kutakuwa miyeyusho tu kwake, maana wale washaharibikiwa...atachofaidi ni adventure tu!!

Kuna ndugu yangu alikuwa kaoa halafu kaenda ishi huko, last two years karudisha mpira kwa kipa, hali mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Angeenda kampala UG kwa kupitia Arusha, Namanga, Nairobi, Kisumu, Busia, Jinja, Kampala.

Ila kwa wenzetu basi ni 24/7, hakuna kulala.

Nilipanda basi Jinja saa 10 jioni, saa 1 asubuhi tuko Namanga
 
Dar - Iringa 4.5hrs, distance 490km approx
Iringa - Mbeya 3 to 3.5hrs, distance 334km approx
Muda ni usiku, gari engine ni V6/V8 (gari nyingine hizi zenye engine za kawaida ni 9 to 9.5hrs)
Dar to Mbeya, vituo vya mafuta ni viwili (Mikumi na Makambako)
Min speed 120kph na mwendo huu ni hadi kule Iyovi, Max speed kisahani chote sehemu zinazoruhusu kama Ruaha Mbuyuni, Makambako hadi Iringa, Moro hadi Chalinze, sehemu kama Mikumi unajitoa ufahamu ile 50kph yao ya usiku unafanya kama huijui...

Sehemu speed kidogo inapungua Kitonga wakati wa kupanda approx 70 to 80kph...

Chimala hadi maeneo ya Nsonyanga Mbeya sababu ya barabara ina madimbwi na mashimo...

Mlandizi hadi pale mbele kidogo ya daraja la juu la treni, barabara ina mawimbi hatari...

Hii ilikuwa achieved wakati hapo Picha ya ndege hawajabomoa barabara, Kingolwira/Kingolwira Magereza hawajaanza chimba barabara, Iyovi hawajaanza kupanua barabara...
Pale mikumi hatari sana kukatiza kwa speed zaidi ya 120

Wanyama ni wanyama tu

Unaweza kuona peupeee mara pAAAp, tembo anavuka, ama nyumbu, ama Nyati (sipati picha)
 
Wakuu ahlan wasalan!!
Nje kidogo ya mada nilikuwa naomba kujua utaratibu wa kuingia nchi jirani kama kenya na chombo binafsi cha usafiri kipi/docx gani natakiwa kuwa nayo zaidi ya ppt. Mwenye uzoefu hasa wa border ya holili/tarakea shukran
 
Kuna siku nilitoka Dodoma saa 2 usiku saa 9 tukaingia Mwanza, moja kwa moja the cask. Na palikuwa pamewaka vibaya mno.
The cask huwa kina waka sana.. kipindi cha nyuma kila weekend ilikuwa lazima niwepo pale.. naanzia alhamisi,.ijumaa hadi jumamosi.. naondoka jumapili 😀😀😀😀.. ila sasa hivi majukumu mengi sana
 
The cask huwa kina waka sana.. kipindi cha nyuma kila weekend ilikuwa lazima niwepo pale.. naanzia alhamisi,.ijumaa hadi jumamosi.. naondoka jumapili 😀😀😀😀.. ila sasa hivi majukumu mengi sana
Nilivyokuwa Mwanza nilikuwa nakaa sana hapo na pale nyuma villa park I guess kuna samaki na band
 
Wakuu ahlan wasalan!!
Nje kidogo ya mada nilikuwa naomba kujua utaratibu wa kuingia nchi jirani kama kenya na chombo binafsi cha usafiri kipi/docx gani natakiwa kuwa nayo zaidi ya ppt. Mwenye uzoefu hasa wa border ya holili/tarakea shukran
Kadi og na insurance ya comesa I think. Kwa sasa covid 19 negative test certificate
 
Back
Top Bottom