Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kitonga jina kubwa tu ila hamna ishu.

Nyang'oro tamu aisee... nimeshuka na pikipiki mara mbili, nilifaidi sana.

This time nalala na zile kona na miguu minne mpaka nisikie tairi zikilalama
Hahaha mzee wangu anakuambia Kitonga ilikuwa zamani siku hizi ana uwezo hata wa kuendesha pale huku anaongea na simu! Infact watu wengi wanasema Kitonga ilikuwa zamani siku hizi pameboreshwa hata hapatishi sana!

Maana kama kina Sauli na Kilimanjaro pale wanakimbizana na kuovertake utafikiri ni eneo tambarare lenye barabara iliyonyooka kumbe ni mlima wenye kona kali! Maana yake ni kwamba wameshaanza kupaona cha mtoto tu!

Kwanza Nyang'oro mkianza kupapita mnatangaziwa kuwa mnaenda kupita kwenye hilo eneo na mnapewa tahadhari sijajua kama wanafanya hivyo kwenye mabasi yote ya abiria! Ila Kitonga sijawahi sikia tukitangaziwa!
 
Yaani nikiwa zone ile naenda 30kph halafu mtu ananipita mbio nikimkuta mbele anakula cheti najikuta natabasamu....[emoji23][emoji23][emoji23]
Hapo nimeshakula cheti saa ya kwenda na kurudi nikajisahau nikala cheti tena.

Kuna wakati huwa naweka 10k mfuko wa shati. Kwenye kibao najiachia tu. Nampa 10k akikataa namwambia basi andika hiko cheti. Nimeshakuwa sugu wa vyeti sahivi.

Na ukiona traffic analazimisha akupige cheti mjini hapa ujue ametoka maporini. Traffic wajanja wa mjini hawakupigi cheti hata iweje. Hizi 5k na 10k wanachukua sana tu.

Maporini kama huko arusha ndo lazima wakuandikie cheti. Ila mjini 5k unapotea zako.
 
Umeshahu kimoja, wana show hatari ajipange [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…