Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
Hahaha mzee wangu anakuambia Kitonga ilikuwa zamani siku hizi ana uwezo hata wa kuendesha pale huku anaongea na simu! Infact watu wengi wanasema Kitonga ilikuwa zamani siku hizi pameboreshwa hata hapatishi sana!Kitonga jina kubwa tu ila hamna ishu.
Nyang'oro tamu aisee... nimeshuka na pikipiki mara mbili, nilifaidi sana.
This time nalala na zile kona na miguu minne mpaka nisikie tairi zikilalama
Maana kama kina Sauli na Kilimanjaro pale wanakimbizana na kuovertake utafikiri ni eneo tambarare lenye barabara iliyonyooka kumbe ni mlima wenye kona kali! Maana yake ni kwamba wameshaanza kupaona cha mtoto tu!
Kwanza Nyang'oro mkianza kupapita mnatangaziwa kuwa mnaenda kupita kwenye hilo eneo na mnapewa tahadhari sijajua kama wanafanya hivyo kwenye mabasi yote ya abiria! Ila Kitonga sijawahi sikia tukitangaziwa!