Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wanaosafiri wote ni matajiri ila si matajiri wote wana hobby ya kusafiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaosafiri wote ni matajiri ila si matajiri wote wana hobby ya kusafiri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mara ya kwanza ilikua 2004 pale Babati nilikutana na binti wa kicanada wakuitwa Clara, katika story alikua anaelekea kondoa irangi, sasa akanieleza amesave miaka 11 kuja kutembelea Afrika na Tanzania ilikua nchi ya mwisho then arudi kwao, Binafsi nilijifunza kumbe tatizo kubwa laweza kua saving inakua mtihani, lakini pia malengo, tunatofautiana Binafsi napenda safari na nisiposafiri naugua kabisa upweke, na sina kitu naungaunga tu kibishi kama hivo
 
Kwa mfano kuna tours company nyingi zinakuaga na offer kila mwisho wa mwaka, ukiangalia ni bei ndogo kwenda labda Ruaha, au hata kitulo ukashangae maua au uende Rubondo ukachome samaki fresh achana na habari ya roadtrip kweli ukijipanga unashindwa hata hiyo?
 
Huwezi shindwa kama ni hobby. Ila ukiweka upare mbele? unashindwa vizuri.
 
Ni hobby tu si utajiri

Naunga mkono hoja asilimia mia moja, ujue kuna mtu mko age moja yeye ana nyumba hata nne tena ukichek kipato unamshinda kabisa lakini kwa kua anahoby ya kujenga ndio hivo anajikusanya mdogomdogo mara bati, mara mbao kadhaa, mara mchanga huku wewe unajidanganya iko siku utapata pesa nyingi ndio ujenge kumbe ishakua jioni saa moja kasoro
 
Kuna watu hata mlo tu wanaunga,unadhani wanaweza kupata nguvu za kuunga kusafiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndio hua tunafeli lakini hoby na kuchagua vipaumbele ndio maana nchi za watu wanasomo kabisa linaitwa Life Choice, sasa ukijiendea kama bata haijalishi unazo au hauna usiku unakukuta bado uko njiani na safari bado
"Kujiendea Kama bata"

🤣🤣🤣🤣

Kila mtu na vipaumbele vyake nakubali. Kuna wengine kusafiri safiri haiko damuni, huyu mtu hata awe na mapene bado ataona akisafiri let say kuna upotevu ataufanya (muda na pesa)

Kuna mwingine akishika tu pesa yule asharuka magoroto. Hata kama zitaisha, kesho atatafuta nyingine.
 
Kuna watu hata mlo tu wanaunga,unadhani wanaweza kupata nguvu za kuunga kusafiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunarudi kule kwenye priorities.

Hujawahi sikia mtu ni heri ale ugali mchicha ili tu simu yake isiishiwe bundle? Au anapiga pasi ndefu ili ajitimizie kitu flani mbele?

Cha ubishi basi tu'conclude hivi haya mambo ni 50/50. Kuna mwingine anapenda kusafiri ila pesa hana, mwingine anazo ila hapendi. Mwingine anapenda na pesa zake ni ndogo ila atajibana mpaka ajitimizie vile roho inataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…