Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kupakia vichwa huwa kama ka utumwa, unakosa uhuru..
Punguza speed kaka hujabeba gunia za carrot humu...

Punguza sauti ya radio/ mziki

Washa AC jamani joto litatuua

Fungeni vioo upepo unatuumiza

Kama nyimbo zako zenyewe ndio hizo zima Bluetooth yako niwashe hii yangu.

Tunasimama wapi kula jamani we kaka njaa zinauma

Pale Himo hawana vyakula vizuri bana tafuta sehemu nyingine

Tunakula nusu saa na kupumzika. Usituwahishe sana

Nk nk 😂
 
Wewe ni abiria mzoefu?!
 
Naimani kichwa ukiwa wewe.. hutofanya haya
 
Naimani kichwa ukiwa wewe.. hutofanya haya
Kwanini uwende speed ambayo unatingisha mpaka roho yangu nisiseme?

Uweke taarabu/ singeli nisikwambie ubadilishe nyimbo?

U park gari Kilimanjaro restaurant nisiseme? Wakati unajua pale chakula kawaida sana compared na bei zao

Tulipe hela na AC usiwashe? Yan utulishe vumbi na upepo bila wasi?


Hiiiiiii jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…