Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Jana nilipiga trip ya 200km. Changamoto nilizokutana nazo ni 3. Moja, mvua kubwa njiani hadi aliye mbele yako mita 25 humuoni hadi awashe taa. Pili, nahisi vibao vya speed limit ya 50 vimeongezwa. Hutembei hata 120kph kwa dk10 bila kukutana na kibao. Tatu, askari mmoja alitaka kunipa kosa ambalo sijafanya, kwa kusema nime overtake mahali nisiporuhusiwa. Nikakataa na kumueleza mistari ya barabarani ilikuwaje pale nilipo overtake. Akacheki kama gari ina deni, akakuta haina, akaruhusu niendelee na safari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…