Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Penye maungio tunaegemea pembeni mkuu kwenye yale mamikunjo kama kinanda.Kwenye maungio ndio pabaya dereva akiminya breki lazima uyumbe unakutana na bazazi Bluetooth ipo on anakubambia bila kulipa tozo.
Sehemu salama ukakae mbele karibu na dereva.
Ila kuna siku nilikosa sehemu ya kuegemea ,niliyumba sana hadi kijana mmoja akanipa space nikasimama nikamuegemea japo kwa kujibana.
Hii ndiyo sehemu pekee huwa napenda kusimama..naweza hata kulala usingizi pale ..jinsi yale mavinanda yanavyojikunja na kujikunjua huwa najisikia Raha .