Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Gari Yangu - Carlos N Ft. Young Dee & Abbah

Verse 1:
Ayo ni kwa mziki, kwa beat, thabiti na mic,
Wacha niongelee mkoko wangu mimi kwa dhati,
Na siujuitii sijisifii siusifii una impact,
Naupenda nautumia kwenye zangu nyingi project,

Naipenda sana jinsi ambavyo mi inaniprotect,
260 speed yake zaidi ya baruti,
Suzuki Maruti, Fiat, Renault,
Zote haziikuti nduki lake kama Bugatti,

Huikamatii haikamatwi hata na matraffic,
Maana muonekano wa nje kama gari ya escort,
Nyeusi tii, tint tii, mziki hausikiki,
Ukiacha mlango wazi kiki lake kubwa kikiki,

Ina mwendo, urembo, na ulimbo kwa warembo,
Na mtaani ndo maarufu kama "first blood" ya Rambo,
Kwa skendo, magendo, na kubwa yake nembo,
Ni maduaraduara manne lazima tu utageuza shingo,

Ukitaka kuwa na gari yapaswa anasa kuzikana,
Siyo rahisi kama birthday ukiwa na keki tu unafanya,
Kama hauna we mpe Mungu kila jambo,
Kama Alarm ndiyo inakuamisha itege mortuary uone mambo.

Chorus:
Ukiona gari kali hujawahi kuiona basi ujue hii ndo gari yangu,
Yenye mziki mkali ikipita utaguna bass lake hii ndo gari yangu,
Nasema owe ah ah gari yangu,
Owe ah ah gari yangu ×3.

Huu wimbo huwa naupenda sana, hiyo Verse 1 huyo Carlos N anaongelea Audi then inavyoendelea huko kwenye Verse 2 Young Dee anaongelea VW (original) ila kwenye remix huyo jamaa mwenye wimbo (Carlos N) hayupo kwahiyo Verse 1 Young Dee anaongelea BMW na Verse 2 anaongelea VW hatari kabisa.
 
Maliza na Yang dee dogo namuelewa mnoo
 
Major na Luteni kanali wana hela gani bwanaaa weeee [emoji3][emoji3]..
Hahaha wacha tu ijulikane hivyo hivyo kwamba hawana hela! Ila ukweli ni kwamba jeshini officers yaani kuanzia first lieutenant (wenye nyota moja) kibongobongo wanakunja hela ndefu kuliko waajiriwa wengi wa uraiani wenye bachelors na hata masters sembuse hao majors na lieutenant colonels!

Ili kuwadharau inabidi uwe unaingiza hela zaidi ya wanazopata wao kwa mwezi! Ambazo kwa bongo wanaoingiza hizo ni wale wafanyabiashara wenye biashara zinazoeleweka!
 
Hapana sio dharau mkuu, kuna ma major na ma luteni tumekuja waona baada ya kustafuu hadi huruma na wengine wapo kazini wanatia huruma, mashahara haujawai kutosha mkuu wangu, ni wanajeshi wale wenye kujiongeza ndio wanapeta ila kwa mshahara kuna taasisi kibao hapa zinalipa kishara michafu sana wana mabaka baka wakasome
 
Tinted full nasumbuana sana trafic wakuda, nimeipaga M3 gari yote kuanzia mbele .. madirisha yaani huoni ndani usimame popote pale .. trafic huwa wana mind baadhi ila nakomaa nao tu
 
Maliza na Yang dee dogo namuelewa mnoo
Verse 2:
We unaita Volkswagen mi naita Vimba wewe,
Ukipanda funga mkanda afu anza kuringa wewe,
Speed ya mwewe na inafika hapo mbele tu,
So iconic Dar nzima iko yenyewe tu,

Siyo ya mkopo siyo ya baba ni ya kwangu,
Acha waseme nna nyodo bro nimeipata kwa taabu,
Masnicth wanatia adabu wakiona naingia club,
Jinsi imetulia parking basi inavutia ajabu,

Bei ya rims tu nanunua vitz,
Sa nkikupa bei ya mziki utaniona chizi,
Polisi akisimamisha anaomba hadi kupiga picha,
Piga picha baba uende ukavimbe insta,

Gauge haishuki, vioo juu,
Hamna kupanda mamluki ni watu poa poa tu,
Uswazi hunikuti, staki roho juu,
Wasije kukwangua rangi hawajui bei juu.

Chorus:
Ukiona gari kali hujawahi kuiona basi ujue hii ndo gari yangu,
Yenye mziki mkali ikipita utaguna bass lake hii ndo gari yangu,
Nasema owe ah ah gari yangu,
Owe ah ah gari yangu×3.
 
Labda mwenzio anamaanisha kukunja kuanzia M50 kwa mwezi, tukizungumzia hapo hakuna LT wa M50 per month. 🤣
 
Huyu dogo namuelewa. Zamani zamani nilimuelewa sanaaa 🤣
 
Hizo taasisi si ni zile zile zinazojulikanaga siku zote. Lakini wengine wote ni wale wale tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…