Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Al Jazeera, sio ile ya Qatar bali hii ni ya Ruaha Mbuyuni...asubuhi na mapema hata kuku hawajaanza kuchomwa

View attachment 2479903
Picha nzuri mkuu, binafsi pamoja ya kuwa mdau sana wa T1 sijaingia hii pit stop embu Tia nyama zaidi kuhusiana na pit stop hii, je ni bora kuliko ile ya Msolwa?,naona parking ipo ya kutosha, vipi kuna huduma za mabafu, msosi wake (nyama naziogopa sana)
 

Hapo mkuu sana sana kitu cha kula ni kuku wa kuchoma na hiyo huwa mchana mida ya lunch, lakini sasa huwa ni vurugu vurugu sababu ni mida mabasi huwa yamejazana hapo...

Asubuhi mida kama hiyo nimepita utakuta wauza vitunguu tu, mimi nilipita kwenda kupunguza haja ndogo...

Msolwa ni pazuri zaidi sababu kuna utulivu na mostly ni gari binafsi zinapark...ukiacha Msolwa sehemu nyingine nzuri ni Tawaqal Iringa karibu na Asas pale...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…