Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbeya moja.Mkoa gani unaenda? Weka wazi wadau waone
Ngozi nyeusi imezoea kusikia shida tu mkuu hahahaTushazoea mkuu.....
Hii pia inaweza kuwa msaada wa liftMkoa gani unaenda? Weka wazi wadau waone
Hamna kitu kinauma kama kupitwa wakati unafanya ligi!
ila plate number zinakimbia sana aisee sahivi DVA tena 350+
Sometimes ukipata kampani kama hio Raha sana. Anakuwa pace maker wako hamshindani Bali mnafuatanaSaanaaaa ila kuna kamchezo nataka nikafanye barabarani sijapata mtu tuu wa kufanya nae hako kamchezo 😜.
Kuna siku natoka Arusha hadi Dar niliondoka alfajiri hivo barabara ilikuwa nyeupe.
Kufika Mombo nikakuta magari 2 yanaenda kwa kufatana, kama sikosei zilikuwa Brevis na mark X.
Yaani walikuwa wanaongozana kama wapenzi wameachana umbali huohuo hawakaribiani sana hawaachani sana. Akiovateki wa mbele basi na wanyuma anafata, nikajikuta nimeunga msafara wao aiseeh nikaanza kunogewa na mvutano wao.
Kuna muda nikasikia kuchimba dawa nikatamani wanisubiri ila nawaambiaje, nikajibana niongozane nao labda nao watasimama Korogwe waapii wakanyoosha goti daah kufika Segera nikaona isiwe tabu nisijekuchafua siti ya gari.
Kinyongeee nikapaki nikala nikaendelea na safari yangu. Hawakuwa na speed kubwa sana ila hawaachani ile kufatana mbele nyuma mbele nyuma ile ndo niliipenda.
Nilitamani wasimame niwafahamu ila baada ya kusimama sikuwaona tena hadi nafika Dar.
namba yangu si unayo?Imeisha hio...
Hahaha tunajaribu ..... tutapeana updates hapa ...hakikisha its six cylinder kuendelea vinginevyo utapata shida sana njiani .....Duh kudadeki kumbe ka trip kangu kafupi!
Waenda lini?jamani naombeni lift naelekea Arusha though siyo pisi kali