Okay.
Tukio lilitokea kipindi kile mambo ya madawa yameshika kasi.
Jamaa ndio mara yake ya kwanza kupiga safari ndefu. Alikuwa ana noah yake anatoka Moshi. Pale Msata kulikuwa na barrier. Pembeni imepaki landcruiser ya polisi.
Akapigwa mkono kwenye barrier, akasogea kama anataka kusimama, akaamsha. Jamaa wakamuungia na gari yao.
Jamaa alikuwa anaendesha kwa woga. Hakuweza kuwapiga gape. Kila uelekeo anaoenda wapo nae.
Morogoro road yote akawa anaenda fresh. Kufika Mbezi mwisho kulikuwa na traffic anaongoza magari yanayotoka Goba. Akasimama wakamnyaka.
Wakamrudisha Msata moja kwa moja kituoni. Hawakutaka story nae. Kesho yake akaandikiwa kosa ya kusafirisha bangi. Alivyoona polisi akakimbia. Akahamishiwa kituo kikubwa Tanga mjini huko.
Wale jamaa hawana story na mtu. Akakaa huko ndani siku 3. Akapigia simu ndugu zake, kuja kuongea na muhusika mkuu, wakaambiwa bila 10M jamaa hatoki. Na hakuna mjadala. Kosa ni kusafirisha magunia ya bangi na amesimamishwa akakimbia.
Ndio ikabidi wajipigepige na kuuza kiwanja chake huko nje ya mji. Wakaja na 8M cash, ndo kumuomba sana mkuu wa kituo ndo jamaa akaachiwa ila akatakiwa arudi kwenye ile barrier awarudishie hela yao ya mafuta. Washkaji wakataka 500K ya mafuta na usumbufu. Ilibidi atoe.
Baada ya hapo mchezo ukaisha.
Kumbe ile barrier wanakagua magendo hasa madawa.
NB: Kuna siku nilikuwa nasafiri usiku kwenda arusha, nikapita pale barrier karibu na kia, nikamuuliza polisi wakasema wao wanakagua magendo hasa madawa, mirungi na bangi. Kuna barrier nyingine ukipita kiwanja cha ndege kisongo kama unaenda kisongo.
Mpaka leo naheshimu sana barrier. Ukiwaletea za kuleta wanakulaza ndani.