Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kuna mahali nilikutana na post humu ikizungumzia Highway usiku ni speed hasa,
kuna kausingizi kabaya kanaweza kukutoa nje au ukala mzinga wa head collision na mwenzako, lkn wenzetu huko majuu mmoja tu akikwama au ajali barabarani basi wote mnajaa

Kuna mahali nilikutana na post humu ikizungumzia Highway usiku ni speed hasa,
kuna kausingizi kabaya kanaweza kukutoa nje au ukala mzinga wa head collision na mwenzako, lkn wenzetu huko majuu mmoja tu akikwama au ajali barabarani basi wote mnajaa, sijui ni speed kubwa mbele hawaoni au bumps hakuna, ila Barriers zikiwepo wangepona hebu angalia hii clip (si ya kwetu ila tukio lingezuiliaka) samahani kwa bundle kutumika
View attachment 1703362
View attachment 1703363
Kunakucha asubuhi ni zaidi ya magari 50 yamerundikwa kwenye ajali, lkn Berrier au matuta yetu yangesaidia hivyo ukiikuta berrie mahali simama pata maelezo utajiokoa huwezi jua kuna nini mbele
View attachment 1703365

View attachment 1703367
Hii kitu imetokea Texas last week, inasemekana imehusisha magari kama 133, watu 6 wamefariki na wengine kama 65 hivi wamejeruhiwa. Kilichochangia kwa sehemu kubwa hiyo multiple collision ni hali ya barafu katika barabara na that being super highway naona watu huwa wanakiwasha sana so ile hali ya barafu kuteleza ikawaathiri wengi sana. Hata Bongo ni vile tu tuna junctions nyingi nyingi in between hivyo kuhitajika traffic lights etc automatically breaks zinakua nyingi, lakini zipo barabara ambazo ama zina tuta 1 tu kwa kipande kirefu ama hazina kabisa. Nyerere Road kuanzia pale Airwing mpaka unaunga na Bibi Titi na Ali Hassan Mwinyi hakuna tuta lolote mpaka unachukua Bagamoyo Road unafika Victoria ndio wakutana na tuta la kwanza. Sam Nujoma kuanzia Mwenge unaunga na Mandela Road mpaka unaingia bandarini tuta unakutana nalo moja tu pale Mwananchi kukutahadharisha reli inakatiza na ndipo pekee pia penye kibao cha 50Kph. Hapo Dar ipo congested na miundombinu ungaunga mwana lakini barabara hizo mbili watu hutembea kidogo si usiku si mchana. Hali ya hewa imechangia pakubwa sana ktk hiyo athari.
 
Ila Bongo kwa kweli Mungu huwa anatuongoza tu nyakati nyingine, na hizi alama zetu za majani barabarani tena wakati mwingine wayakuta ndani ya umbali mfupi kweli kufikia kilipo kicheche/tatizo mmmh. Moja nishaikutaga Bwawani pale usiku kama saa 5 na ushee hivi nimepandisha tu kuelekea Moro jamaa ndio wametoka kupasuana luckily kuna waliokua barabarani kutahadharisha madereva wengine kwa tochi ili wapunguze mwendo ilisaidia sana ile maana pale wengi huwa wanapanda nayo nzima nzima aisee. By the way nimejifunza nafikiri pia ni muhimu sana kuwa na tochi ya tahadhari kwenye gari aisee sio nyakati zote tochi ya kwenye simu itafaa.
 
Okay.

Tukio lilitokea kipindi kile mambo ya madawa yameshika kasi.

Jamaa ndio mara yake ya kwanza kupiga safari ndefu. Alikuwa ana noah yake anatoka Moshi. Pale Msata kulikuwa na barrier. Pembeni imepaki landcruiser ya polisi.

Akapigwa mkono kwenye barrier, akasogea kama anataka kusimama, akaamsha. Jamaa wakamuungia na gari yao.

Jamaa alikuwa anaendesha kwa woga. Hakuweza kuwapiga gape. Kila uelekeo anaoenda wapo nae.

Morogoro road yote akawa anaenda fresh. Kufika Mbezi mwisho kulikuwa na traffic anaongoza magari yanayotoka Goba. Akasimama wakamnyaka.

Wakamrudisha Msata moja kwa moja kituoni. Hawakutaka story nae. Kesho yake akaandikiwa kosa ya kusafirisha bangi. Alivyoona polisi akakimbia. Akahamishiwa kituo kikubwa Tanga mjini huko.

Wale jamaa hawana story na mtu. Akakaa huko ndani siku 3. Akapigia simu ndugu zake, kuja kuongea na muhusika mkuu, wakaambiwa bila 10M jamaa hatoki. Na hakuna mjadala. Kosa ni kusafirisha magunia ya bangi na amesimamishwa akakimbia.

Ndio ikabidi wajipigepige na kuuza kiwanja chake huko nje ya mji. Wakaja na 8M cash, ndo kumuomba sana mkuu wa kituo ndo jamaa akaachiwa ila akatakiwa arudi kwenye ile barrier awarudishie hela yao ya mafuta. Washkaji wakataka 500K ya mafuta na usumbufu. Ilibidi atoe.

Baada ya hapo mchezo ukaisha.

Kumbe ile barrier wanakagua magendo hasa madawa.

NB: Kuna siku nilikuwa nasafiri usiku kwenda arusha, nikapita pale barrier karibu na kia, nikamuuliza polisi wakasema wao wanakagua magendo hasa madawa, mirungi na bangi. Kuna barrier nyingine ukipita kiwanja cha ndege kisongo kama unaenda kisongo.

Mpaka leo naheshimu sana barrier. Ukiwaletea za kuleta wanakulaza ndani.
Hawa wa barrier ndio polisi ambao niko comfortable nao sana sababu pia hawanaga tamaa za ajabu ajabu. Ni mara chache sana wanaomba hela na hata ukiwapa buku au buku 2 hawanaga noma.

Mitrafiki mishenzi nii hii ya mjini kmmmk. Yani akikupiga mkono ujue anatafta 5-10K ya bure tu...Atakuletea gozi gozi wee.
 
Ila Bongo kwa kweli Mungu huwa anatuongoza tu nyakati nyingine, na hizi alama zetu za majani barabarani tena wakati mwingine wayakuta ndani ya umbali mfupi kweli kufikia kilipo kicheche/tatizo mmmh. Moja nishaikutaga Bwawani pale usiku kama saa 5 na ushee hivi nimepandisha tu kuelekea Moro jamaa ndio wametoka kupasuana luckily kuna waliokua barabarani kutahadharisha madereva wengine kwa tochi ili wapunguze mwendo ilisaidia sana ile maana pale wengi huwa wanapanda nayo nzima nzima aisee. By the way nimejifunza nafikiri pia ni muhimu sana kuwa na tochi ya tahadhari kwenye gari aisee sio nyakati zote tochi ya kwenye simu itafaa.
Last trip from Moshi maeneo flani kabla ya mto wami tu sijui panaitwaje kwa kweli. Tupo ndani ya Altezza 3S. Suka anamwaga moto kweli kweli tunaingia sharp corner moja left & right kuna ngema za kama Mlima umekatwa.
Hamadi kuna jamaa wa Bia kalipigiza container na cabin kati kati ya bara bara. Ngoma imefunga njia.

Sasa kwa yale mazingira nikawa nawaza tu ndio mmeanza ligi maybe mnakimbizana tu. Na pale goma ndio limejiachia mara Tiii... Na wewe unaifata mita kadhaa nyuma kibati uko 160KPH si unaweza kuingia mzima maana lazma kwa ile kona chuma ita Skid.
 
Kuna mahali nilikutana na post humu ikizungumzia Highway usiku ni speed hasa,
kuna kausingizi kabaya kanaweza kukutoa nje au ukala mzinga wa head collision na mwenzako, lkn wenzetu huko majuu mmoja tu akikwama au ajali barabarani basi wote mnajaa, sijui ni speed kubwa mbele hawaoni au bumps hakuna, ila Barriers zikiwepo wangepona hebu angalia hii clip (si ya kwetu ila tukio lingezuiliaka) samahani kwa bundle kutumika
View attachment 1703362
View attachment 1703363
Kunakucha asubuhi ni zaidi ya magari 50 yamerundikwa kwenye ajali, lkn Berrier au matuta yetu yangesaidia hivyo ukiikuta berrie mahali simama pata maelezo utajiokoa huwezi jua kuna nini mbele
View attachment 1703365

View attachment 1703367
Hawa jamaa kilichotokea ni barafu iliganda barabarani hivyo gari zikawa zina loose control. Nadhani unaelewa barafu ikishakuwa kama kioo athari yake kwenye traction ama grip!

Ina maana wanaona mbele kuna mbanga ila wakismash brakes gari zina skid tu mpaka zinaenda kubamiza kilichopo mbele.
 
Hii kitu imetokea Texas last week, inasemekana imehusisha magari kama 133, watu 6 wamefariki na wengine kama 65 hivi wamejeruhiwa. Kilichochangia kwa sehemu kubwa hiyo multiple collision ni hali ya barafu katika barabara na that being super highway naona watu huwa wanakiwasha sana so ile hali ya barafu kuteleza ikawaathiri wengi sana. Hata Bongo ni vile tu tuna junctions nyingi nyingi in between hivyo kuhitajika traffic lights etc automatically breaks zinakua nyingi, lakini zipo barabara ambazo ama zina tuta 1 tu kwa kipande kirefu ama hazina kabisa. Nyerere Road kuanzia pale Airwing mpaka unaunga na Bibi Titi na Ali Hassan Mwinyi hakuna tuta lolote mpaka unachukua Bagamoyo Road unafika Victoria ndio wakutana na tuta la kwanza. Sam Nujoma kuanzia Mwenge unaunga na Mandela Road mpaka unaingia bandarini tuta unakutana nalo moja tu pale Mwananchi kukutahadharisha reli inakatiza na ndipo pekee pia penye kibao cha 50Kph. Hapo Dar ipo congested na miundombinu ungaunga mwana lakini barabara hizo mbili watu hutembea kidogo si usiku si mchana. Hali ya hewa imechangia pakubwa sana ktk hiyo athari.
Bongo sio junctions tu ni foleni nyingi ndo zinasaidia.
 
Last trip from Moshi maeneo flani kabla ya mto wami tu sijui panaitwaje kwa kweli. Tupo ndani ya Altezza 3S. Suka anamwaga moto kweli kweli tunaingia sharp corner moja left & right kuna ngema za kama Mlima umekatwa.
Hamadi kuna jamaa wa Bia kalipigiza container na cabin kati kati ya bara bara. Ngoma imefunga njia.

Sasa kwa yale mazingira nikawa nawaza tu ndio mmeanza ligi maybe mnakimbizana tu. Na pale goma ndio limejiachia mara Tiii... Na wewe unaifata mita kadhaa nyuma kibati uko 160KPH si unaweza kuingia mzima maana lazma kwa ile kona chuma ita Skid.
Sasa hii iwe usiku!
 
Hawa jamaa kilichotokea ni barafu iliganda barabarani hivyo gari zikawa zina loose control. Nadhani unaelewa barafu ikishakuwa kama kioo athari yake kwenye traction ama grip!

Ina maana wanaona mbele kuna mbanga ila wakismash brakes gari zina skid tu mpaka zinaenda kubamiza kilichopo mbele.
Black ice hio isikie tu...
 
Hii kitu imetokea Texas last week, inasemekana imehusisha magari kama 133, watu 6 wamefariki na wengine kama 65 hivi wamejeruhiwa. Kilichochangia kwa sehemu kubwa hiyo multiple collision ni hali ya barafu katika barabara na that being super highway naona watu huwa wanakiwasha sana so ile hali ya barafu kuteleza ikawaathiri wengi sana. Hata Bongo ni vile tu tuna junctions nyingi nyingi in between hivyo kuhitajika traffic lights etc automatically breaks zinakua nyingi, lakini zipo barabara ambazo ama zina tuta 1 tu kwa kipande kirefu ama hazina kabisa. Nyerere Road kuanzia pale Airwing mpaka unaunga na Bibi Titi na Ali Hassan Mwinyi hakuna tuta lolote mpaka unachukua Bagamoyo Road unafika Victoria ndio wakutana na tuta la kwanza. Sam Nujoma kuanzia Mwenge unaunga na Mandela Road mpaka unaingia bandarini tuta unakutana nalo moja tu pale Mwananchi kukutahadharisha reli inakatiza na ndipo pekee pia penye kibao cha 50Kph. Hapo Dar ipo congested na miundombinu ungaunga mwana lakini barabara hizo mbili watu hutembea kidogo si usiku si mchana. Hali ya hewa imechangia pakubwa sana ktk hiyo athari.
Ila angalia magari 133 wamefariki watu 6, Sisi hapo zingeumana buses tano tu tungezika 200!
 
Hawa jamaa kilichotokea ni barafu iliganda barabarani hivyo gari zikawa zina loose control. Nadhani unaelewa barafu ikishakuwa kama kioo athari yake kwenye traction ama grip!
Ina maana wanaona mbele kuna mbanga ila wakismash brakes gari zina skid tu mpaka zinaenda kubamiza kilichopo mbele.
Udereva kazi ngumu sana na inahitaji uzoefu
kuna Kiongozi tumempoteza wamemzika jana Kigoma
wanashuka mteremko wa Nzuguni wameongozana vizuri na speed wanafika nane 8 Stand ya Mkoa jamaa akachomekewa gari mbele ya Harrier yake, jamaa akaona isiwe tabu akafunga breki Harrier ikateleza /skid akitaka kuovertake Lori inakuja na foleni kibao, kwa vile gari ilishakata barabara , nyuma ilifuata Noah ambayo ilimgonga ubavu wa Harrier ambapo dereva alikuwepo, ndipo ikawa chanzo cha kifo
na hapo palikuwepo kamvua / manyunyu
 
Dah apumzike kwa amani.
Ila barabarani bhanna, hakunaga,mzoefu kila siku watu tunajifunza kutokana na makosa yetu wenyewe au ya madereva wenzetu. Cha msingi ni kuzingatia udereva wa kujihami tu na Mungu akusimamie
 
Hio barafu ya kioo inatesa hata watu wa kupanda mlima huwa wanapambana isije jua ikawaka hujatoka kileleni maana hutashuka. Utateleza na kujibamiza kwenye mimawe mpaka umauti utapokufika. Hio barafu ni msala sana.
Kuna mshikaji wangu ilitaka kumuua hio black ice motorway. Alikuwa 5series alispin mashine ikaflip ikalala chali. Mafuta yanamwagika kabanwa hawezi kutoka.
Sheria za wazungu hapo hammna mtu kusogea mpaka fire brigade waje wamtoe. Alijikuta yuko hospitali tu maanake alikata moto wakati anasubiri fire brigade waje. Alivyopona aliuza 5series.
 
Back
Top Bottom