Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Chanzo, nahisi.. kuna sehemu nilipiga shimo ikapata pancha ikawa inatoa mdogo mdogo, na sikuwa nimejua + mwendo kasi 220, 240 to 260.. + lasta . Ila sina hakika 100 hizo ni hisia tu. Bridgestone ni tire bora kabisa tena sana. Umbali ni kama mita 200.. maana ilikuwa kwenye 260 mda huo.. nashukuru Mungu, alinijalia kuwa mtulivu hadi naenda paki
Un even road surface ndio chanzo kikubwa cha tyre blowout hasa katika speed hizo kubwa
Tanzania hatuna barabara nyingi standard ,nyingi zimeungwa ungwa na zina matuta au rasta ambazo hazina kiwango. mnapo practice hizo speed kali kali at leats wekeni akiba ya hilo.
Uzuri pia ulitumia Tairi za uhakika, wazungu wana kitu kinaitwa fail safe , your blowed tyre just did that , ingekuea tairi ya kichina hapo unagepata na fair amount of damage kwenye gari pia , hazilipukagi kwa format nzuri
 
Pale opposite na kitete hospitali wanapika mchemsho wa kuku wa kienyeji unaitwa 'Abuja'.

Mzito kama roast, una hoho kibao unakuwa wa kijani kinyama. Ladha ya kipekee sana. Ndio kitu unique kuhusu Tabora, sijaona pengine.

Ila pisi za hii town ukiwa viwanja zina shobo hatari. Zinajirahisisha balaa. Kukufuata kukuomba uwanunulie bia sio ishu sana. Ukisalimia tu unaombwa bia.

View attachment 1815900View attachment 1815901
Panaitwa PPP a.k.a Triple P hatari sana hio Abuja
 
Hahaha mzee wangu anakuambia Kitonga ilikuwa zamani siku hizi ana uwezo hata wa kuendesha pale huku anaongea na simu! Infact watu wengi wanasema Kitonga ilikuwa zamani siku hizi pameboreshwa hata hapatishi sana!

Maana kama kina Sauli na Kilimanjaro pale wanakimbizana na kuovertake utafikiri ni eneo tambarare lenye barabara iliyonyooka kumbe ni mlima wenye kona kali! Maana yake ni kwamba wameshaanza kupaona cha mtoto tu!

Kwanza Nyang'oro mkianza kupapita mnatangaziwa kuwa mnaenda kupita kwenye hilo eneo na mnapewa tahadhari sijajua kama wanafanya hivyo kwenye mabasi yote ya abiria! Ila Kitonga sijawahi sikia tukitangaziwa!

Nilipita pale na mtu asiee anaovertake hapa na hapa
Nilifika Iringa nimeloa jasho

Halafu anakuambia “si ulale “[emoji28]
 
Mzee unapiga roadtrip si mchezo! You are my role model!

Mimi nimewahi kupiga roadtrip za siku kadhaa mfululizo mara mbili tu na zote ni za kikazi tu! Ya kwanza ilikuwa Dar-Tanga-Kilimanjaro-Arusha. Ilikuwa ni safari ya usiku na mchana hakuna kupumzika na haikuwa safari ya moja kwa moja bali tulipitia kwenye wilaya kadhaa safari ilianzia Dar jioni via Bagamoyo, tukaingia Msata then tukaingia Tanga.

Tanga tulipitia wilaya za Korogwe, Handeni, Muheza, Pangani na Tanga mjini. Kilimanjaro tuliingia Mwanga ndani ndani, Moshi ndani ndani, Hai ndani ndani, na Siha ndani ndani then tukaenda Arusha mjini ambapo ndiyo ilikuwa mwisho wa safari yetu na pale ndiyo tukatafuta hotel tukapumzika.

Maana safari nzima tulikuwa tunalala kwenye gari then tunaamsha, na kulala kwenyewe ni nusu saa hadi lisaa limoja imeisha hiyo, maana tulikuwa watatu including dereva na dereva akawa anatuambia tusilale tumpigishe story ili asije akasinzia akachochora. Yaani tulikuwa tunashuka sehemu kula tu au kuchimba dawa na kuoga kwenye hivi vyoo na mabafu ya kulipia basi so tulivyofika Chuga ndiyo tukapumzika.

Tukajipa siku nzima off ambayo ndiyo tulipanga tulale hiyo siku nzima halafu kesho yake ndiyo tuamshe kurudi Dar. Wenzangu walikuwa wamechoka wakalala kama pono ila cha ajabu mimi kulivyokucha ndiyo kwanza nikawaacha, nikaingia town pale nikazurura kidogo then Baadaye nikaenda Rombo nako nikazurura kidogo hadi jioni then ndiyo nikarudi Arusha, kesho yake sasa ndiyo tukaamsha kurudi Dar.

Ya pili ni hizi za juzi hapa ila hizi angalau zilikuwa siku chache na hazikuwa za usiku na mchana maana tulifikia Mbeya mjini. Jumamosi ilikuwa Dodoma-Mbeya, Jumapili ilikuwa Mbeya-Chunya (kwenda na kurudi), Jumatatu ilikuwa Mbeya-Kyela (kwenda na kurudi) na jana Jumanne ndiyo tukaamsha Mbeya-Dar.

Mimi ninavyopenda safari yaani hata nisafiri vipi huwa niko fresh tu tena kadiri ninavyozidi kusafiri ndivyo ninavyotamani nisafiri zaidi na zaidi nifike sehemu ambazo sijawahi kufika. Yaani nimejigundia napenda sana safari na safari inapoanza huwa sitamani tufike tunakoenda sema tu ndiyo hivyo kazi haziruhusu.

Nawaonea sana wivu watu wanaofanya kazi zinazowalazimu kusafirisafiri kila mara na mimi starehe yangu siyo kuendesha bali kuwa mbele pale pembeni ya dereva mimi ndiyo huwa naenjoy zaidi. Mfano zile safari ambazo mnatakiwa mpeleke mizigo kwenye mikoa mbalimbali halafu mko na cruiser ama coaster wawili au watatu tu dereva na utingo halafu safari iwe day and night yaani huwa nafurahia acha kabisa.

Naamini huu kwangu ni mwanzo tu natamani ifike kipindi nipate safari za mfululizo kama wewe hadi nizikimbie mwenyewe. Halafu mimi sichaguagi usafiri mimi gari, meli, ndege au treni vyote twende tu tena huwa naenjoy slow transports kuliko fast ones mfano meli na treni, unless iwe ni safari ya dharura na haraka ila tofauti na hapo sipendagi haraka kwenye safari zangu, yaani mimi nikiambiwa meli au treni tunayopanda itachukua kuanzia siku mbili na kuendelea kufika tunapoenda ndiyo huwa nafurahia kweli yaani, mradi tu kuwe na basic needs pamoja na some luxuries humo ndani.

Naona naikosea sana nafsi yangu kufanya kazi ya kukaa sehemu moja siku nzima

Am not happy at all

Sijui ntafikia lini kupiga road trips
 
Unatembelea ringi

Hhahaaa hii ilitukuta kijiji cha mwisho kabla haujaingia mafinga kutokea Makambako halafu usiku

Aisee kile kipande kina baridi acha kabisa
Kwenye baridi huwa nawasha heater kama lote 😀😀😀

Tyre ilichanika kama vitambaa na nipo mwisho wa sahani.. haikuwa na namna zaidi ya kutembelea tu
 
Kwenye baridi huwa nawasha heater kama lote [emoji3][emoji3][emoji3]

Tyre ilichanika kama vitambaa na nipo mwisho wa sahani.. haikuwa na namna zaidi ya kutembelea tu

Ile chombo ilikuwa namba B hata Heater haina [emoji23][emoji23][emoji23]

Hapo tushatumia spare tyre

Uzuri mwendo ulikuwa wa kawaida vinginevyo ingekua story nyingine
 
Back
Top Bottom