Kwenye Ship Salvage ambayo sio Contractual waokoaji wanaweza wakataka fidia kuanzia asilimia 10 mpaka 50 sawa na thamani ya Mzigo utakaopona. Wengi hutaka 50% kama alitumia vifaa vyake na watu Kisha akapata uharibifu wa Mali kama boti za uzimaji moto Ili Meli ifike salama bandari.
Hapo wameona Kwa thamani ya Mzigo au nature ya wamiliki wakija kuleta madai ya kupewa asilimia kuanzia 20 mpaka 50 itakuwa ngumu Bora wakae pembeni.
Pia wameona gari zote zilizokuwemo mule lazima msafirishaji alikatia bima(Freight Insurance) hivyo wenye Magari kampuni za bima watahusika kulipa gari zilizoharibika Kwa kipengele Cha Marine Average Law ambapo gari zilizofika salama waliowakatia bima watasaidiana kulipia hasara ya gari zilizoharibika sawa Sawa.
Na mwenye meli akaagiza kikombe Cha Cappuccino akiwa na uhakika meli yake ina ya Hull & Machinery ambapo hapo ana kila sababu ya kulipwa maana moto ni janga ambalo bima Ina cover ( Marine Perils).
Wazee wa ship Salvage kila wakipiga simu na kutuma email hazijibiwi kama Raisi wa Ukraine