Hasa kwa kutembea usiku, ni kichefuchefu.
Jana nimetembea Arusha to Dodoma njia haina matuta ya kipuuzi, njia pana, safi. Kutoka mnada wa nyama pale Dodoma kwenda Iringa hali ikabadilika ghafla utafikiri nimehama nchi nimeingia Sudani.
Hatuna national highyway code ya kuweka utaratibu consistent wa ujenzi wa barabara? Kila mhandisi anajiamulia lake? Matuta hayaongezi gharama za ujenzi? Na zile breki zinazofungwa na heavy trucks linapofikia tuta, hazisababishi barabara kuhitaji kuwa strengthened zaidi ili isitengeneze mawimbi kwenye lile eneo?
Kama unaweka tuta, kibao cha 50 cha nini? Vipi usiku ambapo hakuna pedestrian activity kwenye hilo eneo, hilo tuta lina serve purpose gani?
Mlioshi nchi za wenzetu, wanafanyaje?