Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

kama siku za hivi karibuni umepita mikumi, kona za iyovi, mbuyuni na ilula ukiwa ktk roadtrip, utakubaliana nami kwamba hali safi ya hewa, imefanya natural vegetation ya maeneo hayo iwe na mvuto sana.

embu tazama kipande hiki cha video nilichorekodi juzi nikiwa nashuka mlima kitonga.
View attachment 2522285
Mkuu ilula ni mbali sana na makazi ya watu kama vile yameharibu ule muonekano!

Ukitoka kile kijiji cha mahenge wanachouza karanga barabarani, sogea mpaka ilipokuwa kitonga comfort then sogea tena mpaka pale zege ya mlima inapoanzia..

Hakika hicho kipande kinavutia sana, ni miongoni mwa maeneo machache yanayopendeza sana!!!

Msimu wa mvua, unaweza kuyasikia maji ya mto Lukosi yakiporomoka huko kando ya barabara!!
 
Offroad nazikubali zaidi Landrover 110. Niliwahi kukuta mto umetema huko Manyara gari kibao zimepaki wanasubiri mto upungue.

Kufika pale kucheki maji hayana kasi, nikatia 4wD, Lock diff na Low range. Nikaingia nzima nzima chuma ikaogelea nikatoka upande wa pili.

Jamaa mmoja wa Landcruiser akaona kumbe simple tu nae akafata ila hakutoboa akakaa karibia na kutoka mwishoni.

Ilibidi nirudi tena humo humo kwa reverse nikasimama nikampiga belt na kumkokota hadi ng'ambo. [emoji1373][emoji1373]

Ukiachana na hilo tukio pia kuna sehemu nyingi sana nimewahi kuwakalisha wenye LC's tena kwenye tope ndio usiseme.

View attachment 2522538
Jiandae kushambuliwa na wazee wa mikonga [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Dar Moro wasipofanya kitu kuna siku foleni itakamata watu 48hrs. Kuna siku watu washakaa kuanzia saa4 usiku hadi 11 asubuhi na siku ingine tano usiku hadi 11 asubuhi.
Dawa ni expressway ya kulipia waliyoizungumzia ijengwe na zile njia sita kimara-kibaha zifike Morogoro.
Tatizo wenye maamuzi hawana exposure. Kama imewezekana kujenga sgr inashindikana kujenga proper highway?
Kale kaujenzi pale kwenye mzani wa mikese, kameongeza jam balaa!!
 
Kuna kitu una mtafuta Extrovert ila nakushauri usiyajaribu maji.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mie ni team Toyota chief, ila mziki wa Rover 110 ni habari nyingine kabisa. Landcruiser kamzidi Landrover 110 kwenye durability basiii.[emoji1373]

Ila linapokuja suala la barabara za aina zote Rover ni mfalme tena ukute engine ya diesel (200TDi au 300TDi)
 
Duh GX100 mnyama. Nimepaki karibu mwaka mzima,mvua jua vyote vyake leo nimeitolea uvivu. Nimefanyq service,battery nimeweka mpya. Jina moja chombo imewaka bila misfire yoyote! Mafundi wanang'ang'ania niwauzie! Hapa fundi anatoa matairi nikayajaze upepo kazi iendelee!
Hio mashine ya kwenda. Irudishe road ikapige masafa kidogo.
 
Landrover zile ambazo zinaingiza vumbi ndani na hazina ac zimezidiwa na Land Cruiser kwenye mbio na Luxury. Ila kwa 4x4 ya Landrover ni nzuri. But starting from 2022 hio notion itazikwa na LC300
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mie ni team Toyota chief, ila mziki wa Rover 110 ni habari nyingine kabisa. Landcruiser kamzidi Landrover 110 kwenye durability basiii.[emoji1373]

Ila linapokuja suala la barabara za aina zote Rover ni mfalme tena ukute engine ya diesel (200TDi au 300TDi)
 
Mkuu ilula ni mbali sana na makazi ya watu kama vile yameharibu ule muonekano!

Ukitoka kile kijiji cha mahenge wanachouza karanga barabarani, sogea mpaka ilipokuwa kitonga comfort then sogea tena mpaka pale zege ya mlima inapoanzia..

Hakika hicho kipande kinavutia sana, ni miongoni mwa maeneo machache yanayopendeza sana!!!

Msimu wa mvua, unaweza kuyasikia maji ya mto Lukosi yakiporomoka huko kando ya barabara!!
upo sahihi ndg yangu.
 
Back
Top Bottom