Nina likizo mwezi wa 7 au wa 8 nataka road trip ya siku 5-6 (wiki moja).
Budget imenibana, Pamoja na mafuta (ukitoa service ya gari kabla sijatoka) iwe kati ya 750-900k hivi.
Sasa nina route mbili, moja ya kusini na kati na nyingine ya pwani na Arusha Arusha hivi.
Route ya kwanza:
View attachment 2610769
Hiyo Naanzia Dar to Kilwa Masoko. Nalala Usiku wa kwanza. Kesho yake natoka Kilwa naenda Lindi (Hapa Silali), kisha naenda NDANDA (Naweza kulala au kutolala).Siku ya tatu naenda SONGEA (Nalala) Kisha Makambako na Iringa silali naweza kulala Moro au nikavuka Dar. Jumla approximately kilometa 2000.
Route ya Pili.
View attachment 2610770
Hii ni nyepesi. Natoka Dar to Tanga. Nalala. Najua ni karibu ila nataka niende AMBONI CAVES na kama muda utaruhusu nitaenda MAGOROTO (bila gari nitaiacha Tanga).
Nikitoka Tanga nitaenda LUSHOTO hapo nitalala. Kesho yake mchana nitaenda MOSHI na ARUSHA. Kisha nitarudi Dodoma then Moro Dar.
Hii jumla kilometa 1700 hivi.
Sehemu nilizoweka herufi kubwa sujawahi kwenda au nilienda zamani sana zaidi ya 6 years+ kwahiyo nategemea kuzurura sana.
Vipi nime design vizuri according to my budget?
Nitajitahidi kulala sehemu affordable ili kuendana na budget, nitakua mwenyewe, nikifika mkoa usika muda mwingi nitakua nazurura bila gari ili nione mji na kusave wese pia.
Ushauri kwa wazoefu.