Wazee wa Tanga kusoma albadir kwa waliomuua Mzee Ali Mohamed Kibao

Ila kama inafanya kazi naona Albadiri isomwe tu ili waovu wapate haki yao. Hata kama kuna mshirikina mwenye uhakika na kazi yake tupo tayari kumlipa ili mradi waliofanya unyama wakione cha moto. Pata picha ni baba yako kashushwa kwenye basi ili kwenda kuuliwa? Ungejisikiaje? Binafsi kuna mama jirani alimlaza mama yangu selo kwa ugomvi wao hadi leo sijawahi samehe... Mama yangu na huyo mama washasameheana kitambo mno na ni marafiki ila mimi nimemtakia mama yangu mimi nitaendelea kumchukia huyo rafiki bila kujali kuwa wamepatana. Mzazi anauma mno.
 
mimi ni mwenyeji wa kusini kwahiyo naijua iringa, njombe, makete..e.t.c kusema ukweli kule kwenye swala la kumtoa mtu roho kishirikina kwa watu wauaji kama hao ni rahisi sana haipiti wiki mnaanza kuokota watu walioshiriki. Sijajua kwa upande wa Tanga kitu ikisomwa leo itachukua muda gani tuone matokeo.
Naitaji kuona watu hawavuki hii wiki mambo ya mwezi hayo ni mbali.
 
Hiyo albadir inakuwa na nguvu hiyo kweli au ndio imani hizi hizi za kulishana upepo?
 
Jidanganye,kuna baadhi ya vichaa humu mitaani ni matokeo ya albadir
Hizi story nazifananisha na ile story ya vita vya majimaji kuwa risasi zitageuka kuwa maji. Nasikia kipigo walipata wahehe hakijawahi kutokea. Sijawahi kuamini huo utapeli.
 
Naomba kujuzwa,huo ushirikina unaousema huwa unaletaga matokeo chanya??
 
Alibadili ilisomwa dunia nzima na waislamu siasa kali dunia nzima kuwa askari wa Israel wafe bila kunya wala kujamba na Hamas washinde vita hamna kitu

Hamas wako hoi
Tusubiri upelelezi vyombo vya usalama watupe majibu
.
 
Hiyo albadir inakuwa na nguvu hiyo kweli au ndio imani hizi hizi za kulishana upepo?
Hiyo haina masihara huwa haikosei kama atakayeisoma ni kweli ni mtaalamu achilia mbali na matapeli wa mjini wanaojifanya wanaijua kuisoma ili wapige hela.
Hiyo ni tofauti kabisa na mambo ya tunguri yenyewe inatenda haki kwa kumchagua kila aliyehusika na jambo ambalo limenuiwa na ikitumwa hairudi nyuma na haina tiba.
 
Hamna kitu, utapeli mtupu.
 
Ndio tunautaka huo ushirikina. Huo mnyororo wote ukaokote makopo. Walioua na kupanga njama. Kwa tanga, jamaa wameingia cha kike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…