Ila kama inafanya kazi naona Albadiri isomwe tu ili waovu wapate haki yao. Hata kama kuna mshirikina mwenye uhakika na kazi yake tupo tayari kumlipa ili mradi waliofanya unyama wakione cha moto. Pata picha ni baba yako kashushwa kwenye basi ili kwenda kuuliwa? Ungejisikiaje? Binafsi kuna mama jirani alimlaza mama yangu selo kwa ugomvi wao hadi leo sijawahi samehe... Mama yangu na huyo mama washasameheana kitambo mno na ni marafiki ila mimi nimemtakia mama yangu mimi nitaendelea kumchukia huyo rafiki bila kujali kuwa wamepatana. Mzazi anauma mno.