Wazee wa Tanga kusoma albadir kwa waliomuua Mzee Ali Mohamed Kibao

Hio dua lazma kwanza msomaji awe msafi kwelikweli, na iliwezekana sana enzi hizo kwa sasa labda waroge ila kukuta mtu msafi wa kukusomea albadili ikafanya kazi kwa sasa ngumu
Nilishuhudia hii sehem aisee watu walidondoka kama kuku
 
Comment nzuri sana hii👆🤝
 
Waarabu wanaouawa ni waislam kwa wakristo kwa wapagani.
Na lile ni jambo la kidiplomasia usivichanyane mkuu.
Kuna diplomasia ya kuuwana,
Hizo Dua zenu ni upuzi TU, badilikeni
 

Acha tu ndiyo maana nikawaambia kama hawaamini haya mambo watembee na mke wa mpemba.
 
Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili), simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma.

Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake.

Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe.

Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani".

Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!!

Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."Kama tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!"

FUNDISHO

Usiunge mkono uovu leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, pengine kesho inaweza kuwa zamu yako.!!

Nafikri tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…