Wazee wa Tanga kusoma albadir kwa waliomuua Mzee Ali Mohamed Kibao

Wazee wa Tanga kusoma albadir kwa waliomuua Mzee Ali Mohamed Kibao

Achana na albadiri, wangepiga Ile ya Mkungu wa ndizi. Ndizi moja ikianza kuiva mtu mmoja aliyehusika ni safari
Hio wanawezaga wapemba. Jamaa aliokamata samaki anaambiwa kama ambavyo wanaoza basi na yeye anaoza🤣
 
Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili), simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma.

Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake.

Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe.

Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani".

Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!!

Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."Kama tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!"

FUNDISHO

Usiunge mkono uovu leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, pengine kesho inaweza kuwa zamu yako.!!

Nafikri tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu.
Hadithi yako nzuri sana nimeipenda nitaikopi na kushea.
 
Kutoka Tanga inaripotiwa kuwa wazee wa Tanga wamepanga kusoma dua ya kushitakia almaarufu kama albadil kwa walioshiriki kumuua mzee mwenzao Alli Mohamed Kibao.

Watakaosomewa duwa hiyo ni wale waliopanga njama za maauaji,walioshiriki kumteka,waliomuua,waliofahamu mpango mzima wa mauaji hayo,nk

Kwenye suala la duwa ukiondoa wazee wa Pemba basi wanafuata wazee wa Tanga

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
What comes around goes around
 
Na ninachowapendea Waislamu katika hii Dua yao huwa haitanii na taratibu naanza kuona huenda kuna Watu watapukutika kwa wingi ndani ya Wiki Mbili zijazo hadi Mwezi na si ajabu hata wengine nao Kampeni Ijayo wakawa si Wao kwakuwa watakuwa Wehu na Mburundi kupeperusha Bendera ya 2025 -2030.

Kudadadeki Shikamooni Wazee wa Mkoa wa Tanga. Naona kuanzia sasa Safari za Kisiwani Kuungama hazitopungua.
Inanikumbusha ukimwaga ugali mwingine ana mwaga mboga
 
Alibadili ilisomwa dunia nzima na waislamu siasa kali dunia nzima kuwa askari wa Israel wafe bila kunya wala kujamba na Hamas washinde vita hamna kitu

Hamas wako hoi
Tusubiri upelelezi vyombo vya usalama watupe majibu
.
Wewe umechanganya hiyo dua wanayoisomaga watu wengi tena kwa matangazo ile sio Albadiri kuna jina lake lingine.
 
Kutoka Tanga inaripotiwa kuwa wazee wa Tanga wamepanga kusoma dua ya kushitakia almaarufu kama albadil kwa walioshiriki kumuua mzee mwenzao Alli Mohamed Kibao.

Watakaosomewa duwa hiyo ni wale waliopanga njama za maauaji,walioshiriki kumteka,waliomuua,waliofahamu mpango mzima wa mauaji hayo,nk

Kwenye suala la duwa ukiondoa wazee wa Pemba basi wanafuata wazee wa Tanga

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Je, kama ataonekana aliyeshiriki ni mwenye hadhi serikalini itakuaje na unakuta ndiye anashinikiza uchunguzi piaa😥
 
Back
Top Bottom